Kuna taarifa zilizonisikitisha kidogo hivyo naomba kwa mwenye maelezo zaidi anielimishe.Wanafunzi wa shahada za sayansi waliosoma UDOM na kuhitimu mwaka jana wanapata shida wanapohitaji vyeti vyao,hii imetokea baada ya kuambiwa wanatakiwa kulipa kiasi cha shillingi milioni moja.Kwa maelezo niliyoyapata toka kwa mmoja wa wanafunzi hao anadai kuwa wao walidhaminiwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu(HESLB) na chuo kikatuma taarifa za madai ya ada kwa mwaka wa pili na watatu kama shillingi laki saba kila mwaka.HESLB wakalipa fedha hizo kama chuo kilivyo elekeza,baadae chuo wakawaambia bodi kuwa walikosea ada sahihi ilikuwa sh.milioni moja na laki mbili kwa mwaka,HESLB wakakana madai hayo na wanafunzi wakaendelea na masomo bila kusumbuliwa.Sasa imefika wakati huu ambapo wahitimu hao wanahitaji vyeti vyao,chakushangaza eti wanaambiwa wanatakiwa kulipa hiyo sh.millioni moja,vinginevyo hawapewi vyeti hivyo.Je unashauri nini kifanyike kuwasaidia wahitimu hawa maana kwa mtazamo wangu nadhani wao chuo wanatakiwa kumalizana na HESLB.Miliioni moja kwa Mtanzania wa kawaida si kiasi cha kukipata kilahisi,maana mfanyakazi wa serikari tuu wa daraja la TGS D ambalo ndo wahitimu wa vyuo wanaanzia anahitaji miezi mitatu ili aweze kupata hicho kiasi.