UDOM kwachafuka kwa maandamano

UDOM kwachafuka kwa maandamano

Mhe. AJAYE

Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
32
Reaction score
6
Kwa taarifa tulizozipata hivi punde ni kwamba ‘wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) wanajiandaa kuandamana kushinikiza kupewa hela zao za mafunzo kwa vitendo’ mtoa taarifa amesema chuo ilishapokea pesa hizo tangu wiki mbili zilizopita lakini mpaka sasa bado wanafunzi hawapewa KUSAINI pesa hizo. Na ukisoma magazeti ya leo tar 27[SUP]th[/SUP] June 2014, moja ya gazeti limeandika “UDOM inarudisha pesa za mafunzo kwa vitendo Bodi ya mikopo(HSLB), gazeti limemunukuu mmoja wa viogozi wakuu wa UDOM, Kwa maana hiyo kuwa ni kweli pesa ipo lakini WATAWALA hawataki kuitoa, Mimi na wewe hatujui ila lazima tujiulize maswali kazaaa
1) 1) Kwanini kila siku UDOM…? ikumbukwe kuwa tar 16[SUP]th[/SUP] june palikuwa na mgomo wa WAHAZIRI wa chuo hichohicho waliokuwa wakishinikza kulipwa hela zao za kusimamia mitihani, mwezi wa 5mwaka huu palikuwa na mgomo pia wa wanafunzi kushinikiza kulipwa pesa zao za CHAKULA na MALAZI.
2) 2) Je? Mkataba wa mkopo ni kati Bodi ya mikopo(HESLB) na mwanafunzi? AMA chuo na mwanafunzi? Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa “Mwanafunzi ndiye aliyeingia mkataba na Bodi(HESLB) na chuo ni kama daraja tu (intermediary) wa kufikisha pesa kwa wanafunzi, swali la kujiuliza kwanini UDOM wamepewa hela za wanafunzi halafu wanataka kurudisha..?
3) 3) Kama wanafunzi walianza kumaliza mitihan yao J3 na wengine wanamalizia leo, je hao waliomaliza J3 wanafanya nini mpaka sasa? Sasa isifike wakati watoto wetu waanze kujiunza kwa sababu ya kuzuiliwa pesa yao halali waliyoingia mkataba na bodi na siyo chuo.
Sina mengi kwa sasa tutakuwa tunapeana taarifa kwa kinachoendelea (up date ya kinachojiri), maana nimepewa News kuwa saa 11:45 jion hii kuna kikao kikubwa UDOM…
 
Waambie waende Bungeni hao Mawaziri woooote wahusika wapo
 
mkuu kilichofanyka wanafunzg wa college of educatio kupitia Rais wa college hyo wameambiwa kesho waende makwao..cha kushangaza college ya humanitia wameambiwa wasubir after 1 week...
 
Poleni sana wanafunzi, kusoma Tz yataka kuwa na moyo kama yatima.
 
Wana ubavu wa kugoma kweli mana wengi ni waoga labda chuo kingne kam wahadhiri wanazungushwa ndo nyie poleni sana hii ndo Tanzania
 
Mi pia ni mhanga wa hili taarifa ambazo sijathibitisha,nimezipata kwajamaa yangu wa BOD nikuwa bado wanaanda hayo malipo
 
hii nchi kuna mahala kuna shida,bod nao wanasema tatizo ni hazina,hawa wat mizigo c waondolewe?inauma sana!
 
Mh Ajaye mi niko COED,tumeambiwa twende ,zikija tutaitwa kusain.ni lin?hicho bado kitendawil sijui tatizo liko wp?
 
tmeambiwa tuondoke hela hakna ila tmeandk account # zetu ili pesa itakapopatkana tuwekew,,,ila cdhan km hela ipo polen kw wanaoenda field ugenini
 
Bryan09,Nikwel tumeitika wito wa rais tumeandika majina,naona kama changa la macho bcz mbona akaunt wanazo.Ukwel no pei
 
huko UDOM inaonekana kuna shida sana kama vile uongozi unekishindwa chuo
 
Mwanzon kulikuwa na taarifa kuwa twende,tutaitwa,mara tena,njon muandike acc no.zen, wakat wanazo !hakuna jipya hapa .
 
Dav22,tatizo siyo chuo mkuu tatizo ni bodi,hata bum la mwisho lilchelewa sana vyuo vyote nafuu udsm na udom liliwah kdog
 
mbona wanangu wa TIA (dar) mwaka wa kwanza wamepewa tena hawana hata hiyo field ? yaan pesa ya bure kabisaaa !
 
Poleni sana, UDSM nimeona tangazo pesa imekuja kwa baadhi ya college, wanaanza kusign juma tatu.
 
What is weakening our education is integration of politics in education to the extreme level in Tanzania. RWANDA is integrating ICT in education but Tanzani every sector is monopolised by politician. Pole sana wana udom nimesoma hapo najua matatizo ya hapo. Ukichukua cheti kuwa umehitimu fanya sherehe kuna misuko suko mingi🙂
 
Udom udom udom!! Jamani au kwa sababu wabunge wako huko? Siasa tupu ila poleni mtapewa tuu hata kama itachelewa
 
COED tukaitwa uwanjani saa 12 asubui tukijua labda neema imekaribia kumbe rhaa..wengine tukadhan lazima tuandamane lakin rais wa college atatuasa turudi nyumbani kwa kigezo cha et pesa ikija tutapewa
CHANGA LA MACHO
 
Mbona college of earth science tushasaini pesa ya field jumatatu ya wiki hii ILIYOPITA kabla hata hatujamaliza UE! tupo makwetu twasubiri pesa ya field tukaripoti tulipopangiwa tar 8 july
 
Back
Top Bottom