Post nyingi za hii thread zimeshikamana na propaganda za ccm za kutaka udom ionekane ni chuo cha ccm.Nilishawahi kusema humu kuwa image ya udom inavyoonwa na wengi walio nje yake.Wengi wa watu hawa wanaamini wanachokisikia na kusoma kwenye vyombo vya habari.Sio kweli kwamba wanafunzi wa udom walimchangia kikwete hela ya fomu ya uraisi.Sio kweli wanafunzi wa udom wamempa shahada JK.Sio kweli kwamba wanafunzi wa udom walilaani kitendo cha wabunge wa chadema kususia hotuba ya kikwete.Sio kweli kuwa wanafunzi wa udom wamewahi kuandamana kumuunga mkono Pinda kuhusu mapambano ya mauaji ya albino.Sio kweli kuwa wanafunzi wa udom walikabidhiwa kazi ya kumtafutia wadhamini mgombea uraisi wa ccm kabla ya kampeni za uchaguzi mwaka huu.Sio kweli kwamba wanachuo wengi wa udom ni wanaccm.Wanayoyafanya yote hayo isipokuwa hilo la shahada ya kikwete ambalo wanafunzi hawahusiki,ni wanafunzi wanachama wa ccm wa udom ambao kwa namna ya ajabu wameendelea kugeneralize ishu zao za kichama huku utawala wa chuo ukifumbia macho.Kuna mtu alishaandika thread humu akielezea hali halisi ya kisiasa udom.Alieleza ukweli mtupu na watu humu waliunga mkono sana tu.Inashangaza leo kutokea hili badala ya watu kuendelea kuamini kuwa udom sio CCMlized kama mnavyojua,mnazidi kukatisha tamaa harakati za vijana wanazozifanya kudhihirisha kwenu kuwa sio kweli mnayo/mliyoamini.Tupo pamoja na nyinyi wana Udom endeleeni kupigania stahili zenu.