hivi udini ni nini hasa, tusiwe washabiki pasipotakiwa ushabiki, ebu mtoa mada tupe mtazamo wako juu ya huo udini unaomaanisha hapa, isije kuwa panapoonekana waislam wengi ndio udini lakini kinyume chake si udini, ninachofahamu ni kuwa udini katika uchaguzi wa wanafunzi udom ulionekana kwa zile college tu zilizokuwa na wagombea waislam wengi wagombea, je huo ndio udini, jamani tuacheni ushabiki na pia tukubaliane katika tofauti zake haina maana kuwa wenye kustahili kushika nafasi ni watu wa upande fulani tu na wengine wakiwepo basi ni udini,
hapohapo udom, jumamosi ya tarehe 21 may pamefanyika uchaguzi wa chama cha wafanyakazi wa vyuo vikuu tawi la udom (thtu udom), viongozi wote 25 kasoro mmoja au wawili tu ndio waislam, na waislam waliogombewa walikuwepo lakini walitolewa au fomu zao hazikupitishwa kwa sababu mbalimbali ambazo ni sababu tu za kuwaengua wasiwe miongoni mwa wagombea je hili nalo mnasemaje ni udini au sio udini, lakini hakuna fujo yeyote iliyotokea wla malalamiko yeyote lakini hali hii ingekuwa ni waislam ndio 20 au japo 10 tu basi lazima kelele za udini na jk zingesikika, ifike mahala jamani tukubali kuwa enzi zile za kudidimizana hazipo tena sote tuna haki na nchi hii.
Kwa picha hii ninachokiona mimi ni kweli udom udini upo na haswa wakristo hawataki kuwaona waislam wakishika nafasi yeyote zaidi wanataka tu wao ndio wawe watawala kama ilivyo mahala pengine pote udsm, tra, etc. Sote tunahaki jamani mtuvumilie kama tulinavyowavumilia ndio tumeanza tu kujitokeza itabidi mzoe nasi tuna haki ya kuwakilisha.