University of Dodoma (UDOM)
Public Institution
- Feb 24, 2024
- 50
- 55
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - (NM-AIST), kupitia Maabara ya Akili Unde Afrika - (AfriAI Lab) kwa udhamini wa Taasisi ya Wahandisi wa Umeme na Electroniki Tawi la Tanzania (Institute of Electrical & Electronics Engineers - IEEE Tanzania Chapter), wameandaa Mkutano wa Pili wa Kimataifa kujadili maendeleo ya Akili Unde katika muktadha wa Kiafrika.
Mkutano huo wa siku mbili kuanzia Julai 22-23, 2026 unafanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ukiwaleta pamoja Watafiti wa Kimataifa, Wanataaluma na Wataalam wa Viwanda kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kuhakikisha ujuzi wa matumizi ya Akili Unde unapatikana katika ngazi mbalimbali za elimu hapa nchini. Amesisitiza matumizi ya Akili Unde yalinde utu wa mtu pamoja na kuchochea upatikanaji wa fursa mbalimbali kwenye jamii.
"Akili Unde inabadili namna ambavyo uchumi unakuwa, taasisi zinavyofanya kazi pamoja na watu wanavyoishi." Aliongeza Prof. Mkenda.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, amesema kama taifa tunapaswa kujikita katika athari chanya za teknolojia mpya zinazoibuka kama vile Akili Unde, kwani zina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi. Amewapongeza kizazi cha (Gen Z) kwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana kutokana na matumizi ya Akili Unde.
Imeelezwa kuwa licha ya Akili Unde kutoa fursa kwa viwanda, biashara ndogo na za kati kustawi, bado kuna changamoto zinazozuia nchi za Afrika kunufaika na teknolojia hiyo kutokana na upungufu wa wataalam na miundombinu, kukosekana kwa data zinazotoka Afrika pamoja na kutowajumuisha ipasavyo wanawake na makundi yaliyotengwa katika utafiti na ubunifu wa Akili Unde.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni: " Kutumia Akili Unde kwa Uchumi wa Kidijitali Jumuishi na Endelevu Afrika."