Udom nakupenda

ndechilio shoo

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2013
Posts
997
Reaction score
365
Tuweke wazi kwamba fitna na Majungu sasa basi hivi kwa nini,mnakuwa na chuki na wivu wa kike, Juu ya UDOM bila kuwa na Ushaidi kamili? Kama unajua umekuja kufanya usahili Udom umekosa nafasi hasa kwa wale wanaotafuta ajira Acha wivu wa kike kwani huna sifa wenzio wamepata,pili kuna kundi kubwa ambalo walifukuzwa chuo mwaka 2010 na wengine 2011 kwa sababu ya Mgomo hasa coz ya Uhusiano wa kimataifa(1R)tatu hili ni kundi ambalo wamekosa vigezo vya kusoma udom tukumbuke kwamba kusoma vyuo vya serikari lazima uwe na division 1 au 11,mfano me nina one ya 7 nimemaliza PUBLIC ADMINISTRATION kwa waliopata nafasi kwa division 111 hii ni kwa sababu chuo cha UDOM bado kinahitaji watu na kila kukicha idadi inapungua kwa sababu ya watu kukosa vigezo stahiki,Ikumbukwe kuwa hazima na lengo ya serikari kuanzisha chuo hichi ni baada ya kuona kulemewa kwenye sector ya Elimu,pili ni kuhakikisha kwamba kila Mtanzania mwenye sifa anapata nafasi kusoma kama nchi nyingine,Nakupenda UDOM
 
Kaka kusoma Udom sio sababu ya wewe kukisifia kwa kila kitu kuwa kiko poa. Udom nimesoma pale 2010-2013 shahada ya ualimu. Ninajua inachangamoto kede kede ambazo chanzo chake ni sirikali kugawa madaraka kisiasa na uswahiba kwa vigogo wa juu wa chuo. Kinaendeshwa kama familia ya mtu. Sina shaka na wahadhiri wala ubora wa elimu, elimu inayotolewa pale ni nzuri, wahadhiri ni 50% wabovu 50% wazuri kwa sababu wanapatikana kwa misingi ya ukabila na udini pia. Kama hutoki makabila matatu au dini x sahau kuwa tutorial udom hata kama una GPA YA 5.0 na uko njema kwenye interview utapigwa chini kwa misingi ya mambo mawili niliyo taja hapo juu. Serikali imepoteza pesa nyingi za walipa kodi kujenga chuo lakini imekipa Management ya ajabu ajabu. Chuo kinasinyaa kina uongozi wa kidikteta bora hata Id Amin dada, wahadhiri hawako huru kuongelea matatizo ya jamii na ya nchi kama ilivyo kwa vyuo kama Udsm, Mzumbe na SAUT! Bora kibinafsishwe pesa zijenge nchi kwa kujenga nyumba za walimu kata zote nchini.
 
yap leteni pia na habari, matangazo juu ya usaili wa mwaka wa masomo 2014/2015 kwa wote wa direct na wa equivalent qualification litakuwa jambo la muhimu zaidi
 
Piga kelele tu halafu utakuja kuishia interview za uwanja wa Taifa.....Kwanini vijana msije UDSM/Muhimbili au SUA?. Ukimaliza na ajira unaikuta inakusubiri uchague
 
Tatizo la Watanzania cjui nini ku compare vyuo wakati kamwe haviwezi kuwa sawa hata criteria za chuo bora tatizo watu hawafahamu just ki apreciate chuo ulichosema basi kamwe vyuo haviwezi kuwa sawa
 
NJALI,hili ni jukwaa huru,weka makabira na hiyo din hapa,ili watu wathibitishe kwenye hawa waloajiriwa mwaka huu!
 
Kama mtoa mada alivosema wanaoponda,ni ama walifukuzwa au waliomba wakakosa,mtu timamu hawezponda UDOM ya leo.LOVE UDOM
 
Ulizabei,hivyo vyuo vina ubora gan wa kuizid udom ya leo?umefanya utafit ktk vyuo vyote hivyo?changia kisomi bhana
 
Ulizabei,najua ww kwanza hujasoma/husomi vyuo hivyo,unaona aib kutaja chuo chako,tumeshawajua . MI NIKO UDOM.Tehetehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…