udom ni janga

udom ni janga

Izzo G

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
414
Reaction score
62
natanguliza heshima za dhati kwa wana jf! kama kawaida ya wana jf huwa panapo tokea jambo ambola sio zuri kupeana taarifa ili tuone jinsi ya kulitatua tatizo! ni wiki ya nne sasa tangu watu wamesaini pesa zao za meal and accomodation hawajaingiziwa pesa hizo tumejaribu kuuliza uongozi majibu yao ni yale yale "msijali pesa tunawawekea wiki ijayo" lakini mpaka leo hakuna kitu. kama mnavyojua ndugu zangu chuo hiki ni cha chama hatuna uhuru wala haki ya kuhoji maana ukijifanya mjuaji radhima utahangamia, vijana wanatia huruma hawana matumaini kauli yao ya mwisho huwa wanasema ahh! tutulieni tu wakipenda kutuwekea sawa wasipopenda haya. kiukweli tunaumia sana ndugu zang hata masomo yenyewe hayapandi njaa inatumaliza pole pole huku wakuu wenyewe wakijali matumbo yao hii ndo udom chuo cha kifisadi chenye mlongo wa kuria, ambacho asilimia kubwa ya wanafunzi ni wale wa kipato cha chini watu wa magwepande ambao machozi yetu uhishia moyoni , uongozi wa wanafunzi umekaa kimya kila siku wanatupa moyo kwa maneno ya siasa , siwezi pinga watu ambao huwa wanaleta maada nakusema kwamba udom sio chuo chenye mlengo wa kuzalisha wasomi bora ila ni sehemu ambapo watu wachache wanatumia njia hii kujilimbikizia mihela!! nawasilisha ndungu zangu huku nikiwa nimekula mlo mmoja tu saa kumi na mbili hatujui kesho tena tutakula nini!!
 
Vijana wamepinda, kwa sababu ya kudesa hawajui hata matatizo wayapeleke wapi. Nani aliwaambia JF wanatatua matatizo ya bodi ya mikopo, na chuo kinahusikaje?kwani hamna serikali ya wanafunzi "wizara" inyoshughulikia masuala ya mikopo na elimu kwa ujumla. Hawa ndiyo tuwategemea kuwa watendaji erikalini mara baada ya kumaliza chuo wasiojua hata kufuata taratibu kutatua matatizo, halafu mbaya zaidi wanakosa uvumilivu na kujihusisha na masula ya wizi-actually ni ukibaka (wizi wa surali zilizoanikwa, simu, fedha, kalamu na hata kandambili). Na wakizipata hizo fedha za mkopo ni matanuzi kwa kwenda mbele, ulevi nk- hapo kaka hakuna lecture mpaka tukiishiwa ndiyo turudi kukopana na jamaa. Rotten:blah::blah:
 
we unadhani wote wakipata hizo hela wanafanyia starehe jaribu kufikiria kwa ubongo bhanaa acha maneno yako ya kejeli na kutuona sisi sote wajinga
 
Poleni, Pia ni vizuri kukieleza chama ambacho kimekuwa kikijisifu kwa uadilifu na usikivu kiwasaidie. otherwise akili vichwani mwenuj.
 
kama kweli mnalala njaa basi andamaneni hadi bungeni, mfunge geti kuu. nawaapia ndani ya siku moja hela zenu mnapowe. haki haiombwi inadaiwa. NENDENI MKADAI KWA VITENDO HAPA JF HAMNA WA KUWASAIDIA.
 
Back
Top Bottom