natanguliza heshima za dhati kwa wana jf! kama kawaida ya wana jf huwa panapo tokea jambo ambola sio zuri kupeana taarifa ili tuone jinsi ya kulitatua tatizo! ni wiki ya nne sasa tangu watu wamesaini pesa zao za meal and accomodation hawajaingiziwa pesa hizo tumejaribu kuuliza uongozi majibu yao ni yale yale "msijali pesa tunawawekea wiki ijayo" lakini mpaka leo hakuna kitu. kama mnavyojua ndugu zangu chuo hiki ni cha chama hatuna uhuru wala haki ya kuhoji maana ukijifanya mjuaji radhima utahangamia, vijana wanatia huruma hawana matumaini kauli yao ya mwisho huwa wanasema ahh! tutulieni tu wakipenda kutuwekea sawa wasipopenda haya. kiukweli tunaumia sana ndugu zang hata masomo yenyewe hayapandi njaa inatumaliza pole pole huku wakuu wenyewe wakijali matumbo yao hii ndo udom chuo cha kifisadi chenye mlongo wa kuria, ambacho asilimia kubwa ya wanafunzi ni wale wa kipato cha chini watu wa magwepande ambao machozi yetu uhishia moyoni , uongozi wa wanafunzi umekaa kimya kila siku wanatupa moyo kwa maneno ya siasa , siwezi pinga watu ambao huwa wanaleta maada nakusema kwamba udom sio chuo chenye mlengo wa kuzalisha wasomi bora ila ni sehemu ambapo watu wachache wanatumia njia hii kujilimbikizia mihela!! nawasilisha ndungu zangu huku nikiwa nimekula mlo mmoja tu saa kumi na mbili hatujui kesho tena tutakula nini!!