Udom waanza kuripoti leo udoso mpo?

Udom waanza kuripoti leo udoso mpo?

Matango

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
535
Reaction score
118
leo mwaka wa kwanza udom wanaanza kuripoti. Udoso mmejipangaje kuwasaidia kama mlivyoahidi. Waliofika tayari chuoni watupe hali halisi mpaka sasa!!!!
 
Mimi nasubiri jibu la swali hili,maana mpaka sasa sijui itakuwaje kesho nitakapofika huko?kwanza sikujui hivyo nahisi nitapigwa pesa nyingi mpaka kufika huko chuoni toka stand,Pia inasemekana husiposajiliwa huruhusiwi kulala chuoni kwahiyo kulala ni GUEST HOUSE tu.SASA TATIZO LINAKUJA MIMI POCKET MONEY YANGU NI NDOGO SANA NITASAIDIWA NA NANI? Ingekuwa vizuri sana kama kaka/dada zetu wakawepo maana tungewaambia hali zetu halisi kiuchumi labda wangetuelewa kwa kutupokea,kutushauri na kutuhifadhi hata kama kwa siri mpaka tutakapokamilisha usajili wetu.NAOMBENI MSAADA WENU WAKUU,IWE "MORAL OR MATERIAL SUPPORT" Nawasilisha!
 
leo mwaka wa kwanza udom wanaanza kuripoti. Udoso mmejipangaje kuwasaidia kama mlivyoahidi. Waliofika tayari chuoni watupe hali halisi mpaka sasa!!!!


Hili swali ni muhimu sana kwangu kujua majibu yake! Nawasubiri wahusika kupata majibu yao
 
Zipo taarifa kuwa msongamano ni mkubwa na taratibu siyo rafiki sana za mapokezi na uhakiki wa vyeti, wanafunzi wanahangaika ! Udoso jitokezeni !!
 
Wale wanaoenda kitivo cha afya na sayansi ya tiba (COLLEGE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCE[chas]) mkifika nitafute niwape maelekezo kwani hata mimi nisingesaidiwa sijui ingekuwaje!
 
Wapeni maelekezo hao wanafunzi wengine hawajui usiku wa leo utapita vipi baada ya kukabidhiwa vyumba. Je huduma nyingineza kijamii kama cafeteria hakuna ????
 
wale wanaoenda kitivo cha afya na sayansi ya tiba (college of health and allied science[chas]) mkifika nitafute niwape maelekezo kwani hata mimi nisingesaidiwa sijui ingekuwaje!

wasaidieni walioripoti leo siyo tu chs na colleges nyingine tunasikia wameingia kwenye vyumba jioni hii baada ya msongamano mkubwa wa kujisajili, wameshinda bila kula na hawajui watakula wapi jioni hii. Kumbuka kuwa week end ni ndefu na ina sikukuu je hizo cafeteria hazipo kazini! Kwanini wapokee wanafunzi ikiwa huduma muhimu kama za chakula hazipo au wanafunzi ndio hawajaelezwa zinapatikana wapi
 
Mbaya kabisa j.tatu,j.nne,j.tano kuna sikukuu.sasa sijui huduma za benki itakuwaje pale Dom
 
Kwa vitivo vya udom vimetawanyika lakini kwa wale vitivo vya afya na elimu, earth na natural science kuna sehemu inaitwa Ng'ong'ona maarufu kama kwa wajasi utapata kila uduma unayoitaji, bahati nzuri vijana wamepitia jkt haitasumbua kwani kuna mwendo kama wa dakika 15 hv. Kuhusu cafetaria aka kwa Mwarabu mpaka wanafunzi wawe wengi si unajua watu wanawekeza mitaji yao.
 
Dah! Nimesikitika kwa kutokuiona hii post mapema.
Social sciences hatuna noma kabisaaaa! Ukiwa na friend wako mbona unakula bata hadi unamaliza pilika zako.
 
Back
Top Bottom