UDOM yaandaa warsha ya Jiofizikia kuimarisha utafiti wa rasilimali asilia

UDOM yaandaa warsha ya Jiofizikia kuimarisha utafiti wa rasilimali asilia

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
UDOM-UPDATE-COESE-LIBRARY-CIVE1.jpg


Ndaki ya Uhandisi na Sayansi za Ardhi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa kushirikiana na kampuni ya “Guideline Geo”, inayoongoza duniani katika suluhisho za jiofizikia za maeneo ya karibu na uso wa ardhi, imeandaa warsha ya siku mbili kuanzia leo Alhamisi tarehe 30 Aprili hadi 1 Mei 2026. Lengo la warsha hii ni kuwajengea uwezo wataalamu katika matumizi ya vifaa vya jiofizikia.

Warsha hiyo inawaleta pamoja wadau kutoka taasisi mbalimbali, ikiwemo Taasisi ya Rasilimali Madini (MRI), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), RUWASA, Wizara ya Maji, na vyuo vikuu. Washiriki watapata fursa ya kujifunza matumizi ya teknolojia katika utafutaji wa rasilimali kama maji, madini, mafuta, na gesi.

CoESE 2 (11 of 35).JPG


Katika siku ya pili ya warsha, washiriki watafanya mafunzo kwa vitendo, yakilenga utafiti wa maji, hatua inayolenga kupata wawekezaji ambao watawezesha uwekezaji mkubwa zaidi kuendelea kwenye eneo hilo na hivyo kuleta manufaa kwa taasisi na jamii kwa ujumla.

Warsha hii inatarajiwa kuchangia pakubwa katika kuimarisha utafiti wa rasilimali asilia nchini, na kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya uhandisi hususani sayansi za ardhi.

CoESE 2 (21 of 35).JPG
 
Ni mafunzo mazuri, je baada ya hapo tutegemee nini? kuwa na visima vingi vya maji na mafuta, au maeneo ya uchimbaji wa madini kuongezeka?, na ongezeko hilo litakuwa ndani ya miaka mingapi? Wengi huwa tunahudhuria mafunzo (input), ila matokeo huwa hayaonekani (output).​
 
Back
Top Bottom