University of Dodoma (UDOM)
Public Institution
- Feb 24, 2024
- 50
- 55
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Ndaki ya Biashara na Uchumi (CoBE), leo tarehe 3 Juni katika Ukumbi wa CT1, kimeendesha mjadala maalumu kuhusu nafasi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) katika kuimarisha miundombinu na huduma za umma ili kufanikisha Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Akizungumza wakati wa kupokea Ujumbe Maalumu Kutoa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Lughano Kusiluka, amesema ni muhimu wananchi na wadau kuelewa dhana ya ubia kwani imekuwa chachu ya maendeleo katika nchi nyingi Duniani.
Mzungumzaji Mkuu wa mjadala huo, Mhe.David Kafulila, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), alisema jukumu la kituo hicho ni kusaidia serikali na sekta binafsi kuandaa na kutekeleza miradi ya ubia kwa ufanisi pasipo kutumia kiasi kikubwa cha kodi au mkopo wa serikali kufanikisha mradi husika.
Pia aliahidi kuimarisha ushirikiano na UDOM kwa kuanzisha programu za ubia (PPP) katika ngazi ya Shahada ya Umahiri na kuandaa mafunzo ya muda mfupi, kwa lengo la kuongeza idadi ya wataalamu na kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika sekta hiyo.
Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Prof. Razack Lokina alisema vyuo vikuu vina nafasi muhimu katika kufanya tafiti, kujenga uwezo wa wataalamu na kusaidia usimamizi wa miradi ya ubia kwa maendeleo ya taifa.
Naye, Rasi wa Ndaki ya Biashara na Uchumi (CoBE), Prof. Ismail J. Ismail, alisema mijadala ya kitaaluma husaidia kuunganisha maarifa na uzoefu wa vitendo katika kutafuta suluhisho la changamoto za maendeleo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji kutoka UDOM, Bw. Costatine Mpanda, amesema kuwa kati ya miradi 11 iliyotangazwa, wawekezaji wawili walifanikiwa kushinda baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa. Aidha, amewahimiza wadau mbalimbali kujitokeza kuwekeza katika miradi tisa ya ubia iliyosalia, ambayo itatangazwa tena katika awamu nyingine.
Mjadala huo uliwashirikisha wanafunzi, wanataaluma na wadau mbalimbali wa kimaendeleo waliopata fursa ya kuongeza uelewa kuhusu sera na mikakati ya maendeleo ya nchi kuelekea Dira 2050.