UDOM yashinda Tuzo ya Filamu Beijing kupitia Mhadhiri wake

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinatoa pongezi za dhati kwa Bw. Suleiman Risasi, Mhadhiri Msaidizi kutoka Ndaki ya Sayansi za Jamii (CHSS), Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari (AMS), kwa kufanikisha ushindi wa tuzo ya Makala Fupi Bora (Best Short Documentary) kupitia kazi yake “The Spirit of the Silk Road”.



Tuzo hiyo imetolewa katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la Beijing, ndani ya kipengele cha Short Film Unit – Best Work in The Youthful China.

Mafanikio haya ni heshima kubwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma, tasnia ya filamu nchini Tanzania, na yanadhihirisha uwezo wa wabunifu wa Kitanzania kushindana na kung’ara katika majukwaa ya kimataifa.



UDOM inaamini ushindi huu ni chachu kwa vijana na wabunifu wengine kuendelea kuzalisha kazi zenye ubora wa hali ya juu na ushindani wa kimataifa.

Hongera sana Bw. Risasi kwa kuipeperusha vyema bendera ya UDOM na Tanzania kwa ujumla.

 

Attachments

  • ec8373eb-85d6-45c8-90c9-14f5b7c995d7.jpeg
    211.9 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…