Pale Arusha Technical College, pamoja na wanafunzi kujifunza ufundi, workshop zao hutumika vilevile kuingizia mapato chuo hicho.
Kiongozi,
Hii dhana kwamba 'tumewasomesha' ni dhana muflis. Kujitapa kuwa umemsomesha mtu ni ulaghai na kutaka kuchukua credit yote bila kujali input za huyo msomeshwa, walimu wake na wengine wote walioweka juhudi ktk kumuelimisha mlengwa. It is just wrong.
Hawajakimbia. Wameenda kujitafutia maisha baada ya kuona nchi yenyewe haina mipango ya kuwatumia. Wanakuacha tu kama kuku wa kienyeji ujitafutie mwenyewe. Sasa ndio hivyo wameenda kujitafutia. Waachwe wajitafutie.
Elezea maana ya dhana hiyo kabla ya kutoa madai yasiyoendana na maana husika! Kumbuka nilisema 'tumewasomesha kwa kodi za wananchi' hivyo dhana ya 'tumewasomesha' inajumuisha jamii nzima wakiwamo wao! Ebo!
Commandante:
Kodi ya wananchi haikusomesha watu. Misaada ya kutoka jumuia za kimataifa imesomesha watu.
Ebo! Kodi ya wananchi itasomeshaje wakati 50% ya bajeti inategemea misaada ya wahisani?
Hata hayo masomo mliyowasomesha mengi yameasisiwa na wazungu. Mikanuni, mifomyula, na mambo mengine mengi yanayofundishwa kwenye fani ya uhandisi, imevumbuliwa ulaya na mizungu. Hata hivyo vyeo sijui vya udokta au uprofesa na vyenyewe tumeiga toka kwa wazungu. Heck...hata uvaaji majoho kwenye mahafali tumeiga.
Zakumi huo upofu wa makusudi sio mzuri. Yaani unawabishia Waingereza wenyewe ambao wanakiri hawakuiendeleza hii nchi ipasavyo. Huku kulia kuliko wafiwa na kusherehekea kuliko maharusi sio kuzuri kabisa. Waingereza walitufanya 'pembezoni' ya Kenya!
Jamani mimi naona aibu na hiki chuo chetu. Nimejaribu kuwaccess baadhi ya potential professors wa engineering hapa chuoni kwetu ambao wanaaccess na foundation mbali mbali kama National Science Foundation Research na Rockefeller Foundation na kuwaeleza matatizo yetu lakini hii website ya COET na UDSM haifunguki kabisa. Wameshindwa kuona kitu jamani mbona website za Mzumbe, Makerere na Nairobi zinafunguka vizuri tu. Halafu sijui hata kama kwenye website zao wanaonesha research ambazo wanafanya. Tunakazania chuo chetu sijui kina rank kubwa Afrika wakati vitu vidogo vinatushinda.........
............. nini hasa kinachokusudiwa kufanywa .....?........
..........
After over three decades of use, the infrastructure and machinery have run down and require a huge rehabilitation and replacement. The College Development Partners who injected huge sums to develop the superstructure, understandably, are not willing to fund rehabilitation and maintenance of the same. This task is supposed to be done by the Government. While we acknowledge the huge budget for personnel emoluments, over the years, the University has been receiving less and less moneys for capital investment and other charges; despite increasing numbers of staff, students and programmes. As a result, the area which has suffered most is Infrastructure Maintenance. As elaborated in the attached Brochure, the infrastructure is in bad state, and we can not let it continue to deteriorate, because this will have far reaching adverse effects to the quality of Engineering Education we
are offering. In the bid to reverse this trend we are launching a "CoET
REHABILITATION AND MAINTENANCE FUND".
...........
Prof. J.H.Y. Katima
PRINCIPAL
Ngoja basi nisiwabishie waingereza. Je waingereza waliacha wahandisi wazawa wangapi Kenya ?
Rejea historia ya Misri na Mesopotamia wewe!
Zakumi huo upofu wa makusudi sio mzuri. Yaani unawabishia Waingereza wenyewe ambao wanakiri hawakuiendeleza hii nchi ipasavyo. Huku kulia kuliko wafiwa na kusherehekea kuliko maharusi sio kuzuri kabisa. Waingereza walitufanya 'pembezoni' ya Kenya!
Inasikitisha sana, anyway, sie ndo wana FoE tuliopigania umoja na undugu wakati wote tukiwa FoE na tukawaambia na wadogo zetu na leo hii natumai bado wana FoE spirit ingawa sasa inaitwa CoET. Mie nitatoa hiyo 30,000 kila mwaka kutoka kwenye kamshahara kangu haka kadogo nakopata. Ninawaita wana FoE wote popote waliopo either TZ au abroad tukiokoe chuo chetu, hakuna mpuuzi anayejiita mwanasiasa kama JK atayeiokoa FoE, jamani tulisolve many problems those times let's get back and solve this, if we begin and make a good move, those corrupt stupids may also change and join us. FoE ni ya wasomi wahandisi sio wasomi wanasiasa waliosahau walitoka wapi na kushabikia CCM tu na kusahau maendeleo kama kina kawambwa na wahandisi wengine walioko bungeni.
I urge you all, come n support our fellow Prof. Mwamila. This time we don need to go to FoE slab but we need to take that money to Mwamila na uzuri yeye si fisadi hatazila hizo pesa. Please I urge u again. Regain our FoE spirit n make a change.
Kuchanga hela wakati mtu hajui once hizo hela zikipatikana zitatumika vipi ni ukichaa, Mbaya zaidi watu wanaomba michango hiyo hauwaamini. Nimesema ya kuwa Prof Katima ni mwenyekiti wa bodi ya EWURA, hii bodi imetumia mamilioni ya shilingi kwa ajili ya vikao na matumizi mengine ya kijinga tuu na Katima ndiye aliyehizisha. Leo hii unaniambia mimi nichange hela yangu wakati najua ya kuwa mwisho wa siku hela hii itakuwa misused.
Tatizo la CoET, kama vilivyo vyuo vingi vya kitanzania , ni siasa. Hebu tujiuylize kitu kimoja nini kimetokea kwa BICO (Bureau for Industrial Cooperation) ? Hiki kitengo kilikuwa kinaingizia chuo mamilioni ya shilingi wakati kilipokuwa kinafadhiliwa na wajerumani. Walikuwa wanatengeneza mashine mbali mbali kama kukoboa , parts za viwandani kuziuza, baada y a kuondoka mjerumani mwishoni mwa miaka ya 90 wakina Katima wameshindwa kuongoza. Vipi kuhusu faculty mbali mbali ka umeme , ujenzi wanfanya reaseach gani ambazo zinalenga katika kutatua matatizo tuliyonayo katika viwanda vyetu leo?
Whaaaat?? Waingereza walitufanya "pembezoni" ya Kenya? What the hell is that supposed to mean? Hiki ndio kila siku ninachokizungumzia hapa....eti Waingereza wanakiri hawakuiendeleza nchi ipasavyo....kwani hiyo nchi ni yao? Kwani walikuwa na duty ya kuiendeleza Tanganyika?
Mimi I don't buy this chicken shit eti oooh Waingereza hawakuiendeleza Tanganyika....that's nonsense and it plays right into the Miafrika Ndivyo Tulivyo concept.
Wenye duty ya kuindeleza Tanganyika na Tanzania ni Watanganyika na Watanzania wenyewe na hivi ndivyo ilivyotakiwa iwe hata kabla ya hao Wazungu kuja.
Safi mkuu, hongera kwa hilo
.. Prof. Mwamila muda wake uliisha na sasa amekuwa appointed kuwa VC chuo kikuu cha Mandela Tz.