UDSM: Hawavumi, lakini wamo....

mwanafunzi anatakiwa alipwe dola 300, lakini wakija mlipa wanampa kwa madafu na wanampa laki 3 tu. badala ya 300X1325 = 397500 (kwa sasa)! Ile change yaani 97500 wanajua wenyewe

Ndo humo humo akina Mangi wanamotokea fikiria wanafunzi wapo zaidi ya 100 atapata kiasi gani? Wao wanachukulia wanafunzi mabogus hawajui rate za dola ndo maana wanawapigia humo humo sasa mfadhili katuma dola wao kwanini wasiwape wanafunzi dola badala ya kujifanya wao ndo wanajua na kwenda kuchange wakirudi utasikia rahi ya leo dola imeshuka sana.
 

Ukiona hivyo ujue huyo anaeomba kupiganiwa haki hajapiga shule mwenyewe kivile. Academics hawako waoga kusema ukweli. Mbona anatia aibu dons wa UD huyo? Anawaangusha hata wanaDaruso wa enzi hizo,hawakua hivyo. May be this is the kind of modernity inayoendelea hapo at the Hill. Msaidieni kama hapawezi aanze zake asiharibu jina. Alumni tunakereka sana kupata news za ajabu ajabu namna hiyo toka kwa msomi wa level ya masters.
 
Mh janami mie nimesoma UDSM tena kwa hizo Scholarships nadhani watu tuwe wakweli. Unapoanza kusoma tu mnasaini mkataba unaoonyesha mtu atalipwa kiasi gani kwa muda gani na akimaliza shule nini kinafuata. Pia kwa kawaida pesa haipiti kwa mhadhiri bali kitengo cha fedha cha school husika. Wao waangalie kwenye mikataba walijaza nini ili waone kulalamika kupo sahihi?
 

Yes the guy is talking 'theoretically' and how about you? do u have anything better in hand? like something concrete?
 
Yes the guy is talking 'theoretically' and how about you? do u have anything better in hand? like something concrete?

i dont see the point either.maybe the guy have seen the audito's report. ^\/^
 
did u sign for a stipend and then only to receive an amount which is less than tht u have signed for?

hivi unaifahamu UDSM or what? mbona hiki kitu cha kawaida? wenyewe kuipata hiyo 'scholarship' ni mbinde, sasa kwa vile wao wameshika mpini wanajiona kuwa wana upper hand kwenye kudermine upewa ngapi hata kama sicho walichosaini...na ndio msingi wa thread hii, si umeona mwenyewe analalamika kuwa anapewa kisichokuwa kwenye makaratasi?

Hili lipo, ukijifanya kulalamika unakuwa sidelined, ndo utaratibu hata makazini watu wanalipwa mishahara isiyokuwa kwenye original document ambazo donor anapewaga kama ripoti!

Mgeni wa nji yetu hii ama vipi?
 

r u sure of ur answer?

i want to hear from a horsemouth.

otherwise i doubt the intelligence of someone who can sign a cheque and get paid less than wht s/he signed for..this could be a sign of wht type of students mr.contena has mentioned earlier.sad indeed.
 

Sio kuhusu intelligence,, ni survival! watu wanaangalia survival yao kwa kucompromise intelligence yao! mkuu kua uyaone...na sidhani kama wanasign check...wanasign whatever they call a contract...
 
hizo degree za vyupi ndio zimeshamiri sasa hv,hao dada zetu toka hapo cjui wanajitengenezea future ipi..
 
Kuna mwingine Kitivo cha sheria anitwa Dr kapu la magamba amempa mdada mmoja makao makuu ya mwajiri wake ni Upanga anaitwa Domoni Mfalme akipambana na kuzuia kwa underware2002! Teh teh teh UDSM we acha tu!
 
Kuna mwingine Kitivo cha sheria anitwa Dr kapu la magamba amempa mdada mmoja makao makuu ya mwajiri wake ni Upanga anaitwa Domoni Mfalme akipambana na kuzuia kwa underware2002! Teh teh teh UDSM we acha tu!


Mkuu,

Sijui ni makengeza yangu - kwa hakika sijaelewa ulichopost hapa!
 

Post hii ya ajabu kabisa. Badala ya kuongelea mada, imeenda kumponda mtu binafsi na kumwita mjinga...duh! Ivi kwenda chuo kuna directly equate to an ability ya kudai haki?
Wewe mpe ushauri jinsi ya kushughulikia tatizo. Na ndio maana limewekwa hapa. Kama wewe unajua sana kudai haki, basi tumia hiyo ability yako kumsaidia mwenzie. Na yeye atakusaidi na uwezo wake binafsi alio nao.


Hao wanadaruso wa enzi hizo walikuwaje? Wangekuwa wanajua kudai haki si system ingekuwa bora sasa ivi. It appears kwanza ndo waliochangia mpaka system imekuwa namna hii, kwa sababu uozo wa nyumba hauanzi leo.
P.S: news gani as an alumni ungependa kupata?
 
Duh kama ni kweli, mbaya sana hii....wizi mtupu. Prof.Mukandala upo?
 

Hapana, huu pia ni upotoshaji. Kuna tofauti kubwa sana kati ya scholarship ya sida/SAREC na mashirika mengine kama DAAD. Moja ya tofauti ni kwamba DAAD wanatoa scholarship kwa mwanafunzi mmojammoja (individual support), wakati sida/SAREC wao wanatoa scholarship kwa taasisi (institutional support) for specific activity. Kwa hiyo hela ya scholarship inatolewa kwa chuo, na chuo ndiyo inaamua kinatoa shilingi ngapi kwa kila mwanafunzi kwa mujibu wa mwongozo uliopo katika prospectus.

Ufafanuzi mwingine muhimu wa kuzingatia ni kwamba kiwango cha pesa kinachoonyeshwa kwa mwanafunzi haimanisha kwamba yote ni kwa ajili ya 'stipend'; katika hizohizo kuna sehemu ina-cover administrative costs, etc. Sasa mambo kama haya wanafunzi wetu wa uzamili wangekuwa wanauliza wangekuwa wanapata ufafanuzi kirahisi kabisa. Sasa kama wanaogopa kuuliza, then ni vigumu sana kujua ukweli watabaki ku-speculate!

PS: Mimi naeleza haya kwa sababu mie pia nilisoma masters yangu kwa scholarship yangu hiyo, japokuwa ilikuwa ni enzi hizo kabla ya hiyo sh 150,000/=. Sisi tulikuwa wafuatiliaji; tulifahamu ni kiasi gani sida/SAREC wanatoa, na kiasi gani kinapaswa kwenda moja kwa moja kwa mwanafunzi (yaani direct student costs)-we got the answers because we did not fear to ask!
 
Kitila,
Kama kila issues zinazokuwa-raised zingekuwa zinapata maelezo kutoka kwa watu walioko jikoni kama haya uliyoyatoa, nadhani tungekuwa tunapata mwanga katika mambo mengi.

Pamoja na maelezo yako mazuri, lakini bado kuna matatizo makubwa sana hapo chuoni (especially College of Engineering and Technology, Faculty of Electrical and Computer Systems Engineering (ECSE) in particular) for graduate students. Kwa nini watu hawa-graduate in time? Kwani taratibu zinasemaje iwapo mtu atapitiliza muda unaoruhusiwa bila kumaliza degree yake? Au ni kwa sababu wanaotoa pesa ni wafadhili?

Na kama wahadhiri husika hawawezi kufundisha hao wanafunzi si bora wafute hizo graduate programs ili waendelee kuzaliza undergraduate degrees tu?

Higher Degrees section: Kulikuwa na mama mmoja hapo anaitwa Macha na msaidizi wake Muhando ... walipaharibu sana hapo. Bado wapo? Maana kama hii idara itakuwa inalega lega, basi ndiyo chanzo cha haya matatizo yote yanayowapata graduate students hapo mlimani.
 


Hamna Faculty of ECSE.Mabadiliko ya muundo wa chuo yameondoa faculties.Ipo idara ya ECSE.Kirefu chake ni Electrical,Computer and Systems Engineering.

Kwanini watu hawagraduate in time?Zipo sababu kadhaa.Nitaeleza zile nilizoshuhudia kupitia marafiki ambao ni victims.

1.Hiyo iliyokuwa faculty imekuwa na tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mrefu sana.Hii imesababisha baadhi ya wanafunzi wa shahada za uzamili kupewa majukumu makubwa.Upo mfano wa mtu aliyelazimika kufundisha kozi nzima mwanzo hadi mwisho(from lecturing,setting up and marking exams to results)

2.Njaa.Supervisors wana njaa....mishahara midogo.Hivyo wanatoa priority kwa consultancies and well funded researches kuliko supervision ya wanafunzi hao.Hili lina uhusiano na 1 hapo juu.Imagine kitivo kina uhaba wa walimu.Waliopo njaa kali.Idadi ya wanafunzi inaongezeka.Wakati huohuo wapo vijana wawili wanafanya masters.......kwanini wasifundishe ili supervisor apate muda wa kukimbizana na vijisenti mitaani?

3.Kutumiana.Yupo mwanafunzi wa masters mzuri.Anauwezo mkubwa.Hakika huyu ni wa msaada mkubwa sana kwa supervisor katika kazi zake be it research,consultancy or teaching.Kumruhusu huyu amalize masters yake mapema kutamkosesha supervisor cheap labour.

Mama Macha yupo.Kwa taarifa yako sasa amehamishiwa huko huko ECSE.Kama unamgwaya huyu usisogee ECSE kabsa ha ha haaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…