UDSM ina upekee gani wa kumtunuku mtu Udaktari wa Heshima kuliko vyuo vingine?

UDSM ina upekee gani wa kumtunuku mtu Udaktari wa Heshima kuliko vyuo vingine?

Mapand

Senior Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
134
Reaction score
202
Kama swali linavyojieleza. Natamani kujua kama kuna vigezo vinavyoidhinisha au vinavyofikiwa kwa chuo kikuu iwe hapa Tanzania au Duniani kote katika kumtunuku mtu udaktari wa heshima.

Nauliza hivyo kwasababu kwa hapa Tanzania kila mara utasikia UDSM imemtunuku mtu fulani udaktari wa heshima na sijawahi kuskia SAUT, MZUMBE au MUST
 
Atakuja mwingine kuuliza mbona hakuna diploma za heshima? Ngoja tusubiri majibu ya watanganyika wenzetu.
 
Chuo Kikuu Huria nchini kimemtunuku shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa, Rais wa serikali ya awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete katika mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
 
Kwann boss? Si ya heshima kiwango cha diploma?
Nikikumbuka shughuli za chuo cha ualimu dakawa pale kilosa,hapana kwakweli ile ni jkt ndogo
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kama swali linavyojieleza. Natamani kujua kama kuna vigezo vinavyoidhinisha au vinavyofikiwa kwa chuo kikuu iwe hapa Tanzania au Duniani kote katika kumtunuku mtu udaktari wa heshima.

Nauliza hivyo kwasababu kwa hapa Tanzania kila mara utasikia UDSM imemtunuku mtu fulani udaktari wa heshima na sijawahi kuskia SAUT, MZUMBE au MUST
Nadhani ni initiative tu na si vinginevyo. Hata SAUT au Mzumbe wangemfikiria mhusika kwa maana ya kutambua mchango wake na kuona anastahili kutunukiwa PhD, na kuamua kumtunuku, wasingezuiliwa. Kwahiyo UDSM haijateuliwa kumtunuku mtu yeyote udaktari wa heshima, bali ni maono ya chuo husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo yako yananifanya niendelee kukuuliza maswali mengi lakini kwa uchache tu;

Je, hivi vyuo vingine tofauti na UDSM(pamoja na vyuo vyake vishiriki) havioni michango ya viongozi au watu wanaojitoa kwa mambo mbalimbali kwaajili ya nchi yetu?
 
Inawezekana vinaona, lakini haviko willing kutunuku. Unajuwa tunatofautiana katika kuadmit pale tunapobaini jambo la kipekee ambalo mwenzetu amegundua au amelifanya na kukubalika kwa watu wengi?

Hii hata huku mitaani ipo sana; unamwona mwenzako kafanya jambo linalohitaji pongezi, lakini hatumpi pongezi hizo! Lakini pia wengine (huku mitaani) hawana hata habari ya kujishughulisha na jitihada ambazo mwenzetu ameonyesha, ni mpaka uwe interested na jambo hilo!

Hili linaenda hadi majumbani kwetu, utakuta mtoto amefanya vizuri sana shuleni, kuliko alivyofanya mara ya mwisho; hapa tunatakiwa kuwapa zawadi watoto hawa ili watambue jitihada walizoonyesha, ili wakati ujao wafanye vizuri zaidi.

Kwahiyo, narudia kusema, kuwa, hii ni initiative kwa chuo husika!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom