Well,
Mwikumwiku.
Wewe unasoma "masters" au "postgraduate" kama sikosei na watu wa masters hapa udsm wamekuwa na
dharau siku zote kana kwamba hawakuwahi kupita kwenye undergraduate level.
Well,binafsi nasoma udsm,niko mwaka wa mwisho chuoni hapa.
Nina kushangaa sana pale unaposema kwamba kuna watu hawajitambui,siwezi kuwasemea lakini naweza toa
mawazo yangu ili atleast ufungue macho yako.
Nikuulize swali dogo sana mheshimiwa,.....
Unadhani kwanini wanachuo hapa udsm wanagoma sana (hata kama ni wawili au watatu)?
Unadhani wanagoma kwa sababu wamevuta bangi au?
Binafsi sijagoma,sikuwepo revolution square,...lakini sikuwa sehemu ambayo kwa namna yoyote ile ingeonesha
kuwa dharau wale wanao goma.
Well,kama hujui kwanini wanagoma,ngoja nikupe historia ndogo,maana nyie mnao "fika juu" hua mnajidai hamjui chini kuna nini.
(Atleast kwa semester hii) mgogoro ulianzia pale baadhi ya watu walio pewa mkopo na bodi kutofikishiwa hela zao kwa takribani miezi
miwili.
Hawa wengi wao (kama 1200) hivi walikua ni first year na wengine walikua continuing students.
Waliomba fedha zao toka utawala (kumbuka bodi ilisema haihusiki na fedha kwani mwaka wa masomo tu unapo anza zinapelekwa vyuoni),..lakini utawala ulijibu kwa dharau kwamba hakuna hela.
Hawa first year wengi kama sio wote wakiwa wametoka kwenye familia maskini kabisa,walikopa toka kwa wenzao mda wote huo.
Walijitokeza watu wachache sana kushinikiza uongozi wa daruso ufuatilie fedha hizo,...baada ya wao (daruso) kuonekana wako
slow pia ndipo ukaanza mgomo pale utawala wa kudai fedha hizo.
Rafiki yangu mmoja alifukuzwa kati ya watu wale 48 walokuwa expelled mwanzoni,...nikupe mfano wa huyu tu alivo onewa.
Alikuwa mwaka wa4 engineering,...na kwakua alicheleweshewa hela,nilimkaribisha kwangu mtaani atleast tushee kidogo nilicho nacho
(nimepanga na ninapika geto,atleast maisha yanakuwa rahisi).
Alienda kudai hela zake kwa bush,lakini aliambiwa kesho inayozaa kesho.
Siku kuna mgomo alikua amelala nyumbani kwani alikua anaumwa kichwa sana.
Siku moja baadae,alipigiwa simu kwamba kuna barua yake kwa dean akachukue,...alipo ifuata ilikuwa ni ya
warning..
Baadae mgomo ulikua wa fujo zaidi,na walipo fukuzwa,hata wale waliopewa warning waliunganishwa ndani yake.(kumbuka huyu alipewa warning kwa sababu walipo enda kufuatilia hela zake,aliambiwa aandike jina ili wafuatilie taarifa zake,wali assume kwamba kwa kuwa alikua ana wasumbua sana kudai hela,lazima angekua kahusika kwenye mgomo).
Kinacho endelea sasa:
Wengi tulijua daruso hawafanyi kazi.
Lakini utaratibu ulibadilishwa wa kufanya vikao vya bunge na badala ya viwili (2) kwa semester
kilifanywa kuwa kimoja.
Jumamosi tarehe 7/01/2012 walifanya kikao cha bunge kilicho halali kwani hadi dean of students alishiriki.
Maazimio ya kikao hicho ilikuwa ni majumuisho ya ushahidi kwamba wanafunzi wale waliofukuzwa asilimia kubwa walionewa.
Kwahiyo,kwakua waliwahi kuandika barua utawala kuwaelezea,utawala wakadai barua hiyo haitambuliki kwani
haijatoka kwenye kikao halali,....(so walikata kikao halali.)
Maazimio yakawa kwamba kama sheria inavodai,juma tatu tarehe 09/01/2012 waitishe kura ya maoni na 2/3 wakiitikia basi
lifanyike shinikizo la kutaka walofukuzwa warudishwe. (sijui lakini 2/3 inakusanywa vipi maana huwezi waweka wanachuo wote kwa wakati mmoja.)
Lakini kabla ya hapo,jumapili 08/01/2012,...prof.Mgaya alitoa barua ya vitisho sana kwamba hakuna kufanya mkusanyiko wowote ule. (
Uonevu mwingine unaanzia hapa,kwanini usiwepo mkusanyiko?tupo iraq hapa ?)
Jana 09/01/2012 waliitisha random kura ya maoni kutaka uungwaji mkono.Matokeo yake kwa kuwa walikusanyika viongozi wooooote.
Raisi na mawaziri wote (13) wamepewa barua ya kuwa expelled leo,kosa? Wamefanya mkusanyiko kutafuta uungwaji mkono.
Tofauti na hao,viongozi wooote wa colleges na schools wamekuw suspended jumla yao 89.
Kosa liko wapi hapa?
Chanzo cha haya yote ni nini?
Wanafunzi walinyimwa hela zao kwa wakati.
Unataka waishi vipi?
Kwanini wakiuliza wanajibiwa upupu eti "hela hamna"?mbona wakigoma hela zinatoka?
Na kwa taarifa yako faculty requirements hua zinatoka semester ya kwanza,hadi leo hii hazijatoka.
Wengi wetu tumetulia tufanye mitihani kwanza kumaliza semester,...lakini ni bomu lingine linalo kuja,...
Kwanini hawaangalii kuziba vyanzo vya vurugu hadi vurugu zitokee ndo wajidai wanajua kufukuza?
Usijidai kwakua una hela za kujisomesha hicho kiji-post graduate sijui ki-masters ndo udhani kila mtu anaweza
kujilipia na kuji support kwa kila hali.
Kama hauwezi kuwa na ubinadamu kidogo sana ni bora ukakaa kimya.