Udsm inaelekea wapi? Barua hiyo soma mwenyewe na utoe maoni yako

Udsm inaelekea wapi? Barua hiyo soma mwenyewe na utoe maoni yako

Tathimini nzuri! Hoja yangu ni kwamba kama kila mwanafunzi wa chuo angejitambua akayajua malengo yake hata kabla ya kuingia chuo, haya yote yasingetokea! Tatizo la kutokuwa na malengo binafsi kwa baadhi ya wanafunzi ndiyo sababu ya baadhi yako kujikuta wanadandia malengo ya watu wengine mwisho wa siku wanajikuta hapo walipo!

Anyway, mimi siyo tu nasoma sheria bali ni mwanasheria.
Hopeless mwanasheria! nyie ndio mnasaini mikataba ya ovyo kwasababu ya njaa zenu. Acha njaa wewe.
 
Ha ha ha ha ! Unaninyanyapaa bure! Kwa hiyo unataka kusema mgomo unamkono wa vyama vya upinzani!!!? Angalia usije ukaharibu zaidi kesi yako mwenyewe!
Kuna mkono wa ccm, maana nyie ndo mnaokalia haki za wanachuo.
 
Hawa wahuni waliochukuliwa hatua watakuja kukumbuka shuka wakati kumekucha.

David Silinde, Kabwe Zuberi Zitto, John Mrema, Mwita Mwikabe Waitara, Julius Mtatiro, nk ni baadhi tu ya wanafunzi waliowahi kuwa vinara wa Migomo UDSM na kupata misukosuko ya kusimamishwa masomo na hata wengine wakajikuta wanasoma miaka minne katika kozi zao za miaka mitatu. Je na hawa vinara wa migomo wa enzi hizo nao utawaita ni Wahuni?

 
Magraduate wa Mzumbe utawajua tu! Pole sana!
Huyo sio wa mzumbe mkuu, usiwasaidie kubadili mada, maana tukianza kushambuliana UD na Mzumbe mada itapotea na wale vibaraka wa ccm watapumua. tuendelee kujadili thread.
 
huyo sio wa mzumbe mkuu, usiwasaidie kubadili mada, maana tukianza kushambuliana ud na mzumbe mada itapotea na wale vibaraka wa ccm watapumua. Tuendelee kujadili thread.

ni kweli tusipoteze mwelekeo wa thread kwa kuingiza mambo ya mzumbe hapa. Kilichopo ni hali ya fukuzafukuza inayoendelea pale udsm.
 
Well,
Mwikumwiku.
Wewe unasoma "masters" au "postgraduate" kama sikosei na watu wa masters hapa udsm wamekuwa na
dharau siku zote kana kwamba hawakuwahi kupita kwenye undergraduate level.

Well,binafsi nasoma udsm,niko mwaka wa mwisho chuoni hapa.
Nina kushangaa sana pale unaposema kwamba kuna watu hawajitambui,siwezi kuwasemea lakini naweza toa
mawazo yangu ili atleast ufungue macho yako.

Nikuulize swali dogo sana mheshimiwa,.....
Unadhani kwanini wanachuo hapa udsm wanagoma sana (hata kama ni wawili au watatu)?

Unadhani wanagoma kwa sababu wamevuta bangi au?
Binafsi sijagoma,sikuwepo revolution square,...lakini sikuwa sehemu ambayo kwa namna yoyote ile ingeonesha
kuwa dharau wale wanao goma.

Well,kama hujui kwanini wanagoma,ngoja nikupe historia ndogo,maana nyie mnao "fika juu" hua mnajidai hamjui chini kuna nini.
(Atleast kwa semester hii) mgogoro ulianzia pale baadhi ya watu walio pewa mkopo na bodi kutofikishiwa hela zao kwa takribani miezi
miwili.
Hawa wengi wao (kama 1200) hivi walikua ni first year na wengine walikua continuing students.
Waliomba fedha zao toka utawala (kumbuka bodi ilisema haihusiki na fedha kwani mwaka wa masomo tu unapo anza zinapelekwa vyuoni),..lakini utawala ulijibu kwa dharau kwamba hakuna hela.

Hawa first year wengi kama sio wote wakiwa wametoka kwenye familia maskini kabisa,walikopa toka kwa wenzao mda wote huo.
Walijitokeza watu wachache sana kushinikiza uongozi wa daruso ufuatilie fedha hizo,...baada ya wao (daruso) kuonekana wako
slow pia ndipo ukaanza mgomo pale utawala wa kudai fedha hizo.

Rafiki yangu mmoja alifukuzwa kati ya watu wale 48 walokuwa expelled mwanzoni,...nikupe mfano wa huyu tu alivo onewa.
Alikuwa mwaka wa4 engineering,...na kwakua alicheleweshewa hela,nilimkaribisha kwangu mtaani atleast tushee kidogo nilicho nacho
(nimepanga na ninapika geto,atleast maisha yanakuwa rahisi).
Alienda kudai hela zake kwa bush,lakini aliambiwa kesho inayozaa kesho.
Siku kuna mgomo alikua amelala nyumbani kwani alikua anaumwa kichwa sana.
Siku moja baadae,alipigiwa simu kwamba kuna barua yake kwa dean akachukue,...alipo ifuata ilikuwa ni ya warning..

Baadae mgomo ulikua wa fujo zaidi,na walipo fukuzwa,hata wale waliopewa warning waliunganishwa ndani yake.(kumbuka huyu alipewa warning kwa sababu walipo enda kufuatilia hela zake,aliambiwa aandike jina ili wafuatilie taarifa zake,wali assume kwamba kwa kuwa alikua ana wasumbua sana kudai hela,lazima angekua kahusika kwenye mgomo).

Kinacho endelea sasa:

Wengi tulijua daruso hawafanyi kazi.
Lakini utaratibu ulibadilishwa wa kufanya vikao vya bunge na badala ya viwili (2) kwa semester
kilifanywa kuwa kimoja.
Jumamosi tarehe 7/01/2012 walifanya kikao cha bunge kilicho halali kwani hadi dean of students alishiriki.
Maazimio ya kikao hicho ilikuwa ni majumuisho ya ushahidi kwamba wanafunzi wale waliofukuzwa asilimia kubwa walionewa.
Kwahiyo,kwakua waliwahi kuandika barua utawala kuwaelezea,utawala wakadai barua hiyo haitambuliki kwani
haijatoka kwenye kikao halali,....(so walikata kikao halali.)

Maazimio yakawa kwamba kama sheria inavodai,juma tatu tarehe 09/01/2012 waitishe kura ya maoni na 2/3 wakiitikia basi
lifanyike shinikizo la kutaka walofukuzwa warudishwe. (sijui lakini 2/3 inakusanywa vipi maana huwezi waweka wanachuo wote kwa wakati mmoja.)

Lakini kabla ya hapo,jumapili 08/01/2012,...prof.Mgaya alitoa barua ya vitisho sana kwamba hakuna kufanya mkusanyiko wowote ule. (Uonevu mwingine unaanzia hapa,kwanini usiwepo mkusanyiko?tupo iraq hapa ?)

Jana 09/01/2012 waliitisha random kura ya maoni kutaka uungwaji mkono.Matokeo yake kwa kuwa walikusanyika viongozi wooooote.
Raisi na mawaziri wote (13) wamepewa barua ya kuwa expelled leo,kosa? Wamefanya mkusanyiko kutafuta uungwaji mkono.

Tofauti na hao,viongozi wooote wa colleges na schools wamekuw suspended jumla yao 89.

Kosa liko wapi hapa?
Chanzo cha haya yote ni nini?
Wanafunzi walinyimwa hela zao kwa wakati.
Unataka waishi vipi?
Kwanini wakiuliza wanajibiwa upupu eti "hela hamna"?mbona wakigoma hela zinatoka?

Na kwa taarifa yako faculty requirements hua zinatoka semester ya kwanza,hadi leo hii hazijatoka.
Wengi wetu tumetulia tufanye mitihani kwanza kumaliza semester,...lakini ni bomu lingine linalo kuja,...
Kwanini hawaangalii kuziba vyanzo vya vurugu hadi vurugu zitokee ndo wajidai wanajua kufukuza?

Usijidai kwakua una hela za kujisomesha hicho kiji-post graduate sijui ki-masters ndo udhani kila mtu anaweza
kujilipia na kuji support kwa kila hali.
Kama hauwezi kuwa na ubinadamu kidogo sana ni bora ukakaa kimya.
Poleni wadogo zangu lakini unaemweleza sio mtu wa kuelezwa haya. wewe unafikiri kuwa anasoma masters sheria; hakuna mtu yeyote anayesoma sheria hapa nchi ktk masters anaweza kutoa maoni kama haya, huyu ni kibaraka wa ccm kajifanya mwanasheria. Usiwachafue masters wote kwasababu ya chizi mmoja.
 
Tathimini nzuri! Hoja yangu ni kwamba kama kila mwanafunzi wa chuo angejitambua akayajua malengo yake hata kabla ya kuingia chuo, haya yote yasingetokea! Tatizo la kutokuwa na malengo binafsi kwa baadhi ya wanafunzi ndiyo sababu ya baadhi yako kujikuta wanadandia malengo ya watu wengine mwisho wa siku wanajikuta hapo walipo!

Anyway, mimi siyo tu nasoma sheria bali ni mwanasheria.

Wewe unazungumza nini. maisha ya sasa pamoja na ubepari bila ya collective responsibility hatutafika. wewe nadhani mtu kama gandi, nyerere, nkurumal wangekuwa wanajiangalia wao leo nchi zao zingekuwa wapi? nyerere hujui aliachishwa kazi sababu ya siasa. gandi na nkurumah wamepoteza maisha sababu ya siasa. sasa kama wewe huoni sababu ya kurazimisha haki itendeke shut up. endelea hapo kusoma na ukatengeneze miswada mibovu na kuwatumikia hao wapuuzii ili mkono wako uende kinywani. huku wajukuu wako wakikuuliza siku umetufanyia nn? ila umeshindwa kwa sababu umi mi wako. kalaghabao.
 
Kama wakuu wa elimu wanaandika barua yote in capital letters sijui tunajifunza nini hapo!!!

sina hakika kama kilichoandikwa hapo ni barua nadhani ni "Tangazo"
 
Ndo tunaanza kuona athari za baadhi ya watu walafi kuhongwa vijisenti na kugawa rasilimali zetu kwa bei ya vitunguu. Tunashindwa kutatua matatizo ya msingi kabisa ya elimu ya vijana wetu tunabaki na frustrations za kuwapiga virungu na kuwatimua. Responsible leadership ilikufa kipindi cha mwalimu, hivi sasa ni selfish leadership. Sioni matumaini ya nchi inakoelekea, labda baadaye hali yaweza badilka. You never know
 
Kinachotokea sasa ni impact za viongozi majuha wa Ccm na vibaraka wao ndo wanaona njia nyepesi ya kuleta hofu kwa wasomi na kuwasuspend ila wafahamu ndo wanapandikiza mbegu za mabadiliko udsm ni sehemu ndogo tu ya watz wanaonewa na kuonekana wahuni mbele ya jamii lakini jamii ikae ikitambua wasomi ndio nguzo ya taifa lolote imara na huu ni mwanzo na fukuto la mabadiliko ya kweli wanaudsm tuungane mikono ktk kupigania haki ya wenzetu inayodhulumiwa na hawa mafisadi and we should rem that if u think about today how about tomorrow after finishing of ur studying (no employment)
 
@mwikumwiku, cdhan kama mtu mzma kwa maana ya uzma na umri atafka chuo kikuu bla kujua lengo lake...tafadhal tusi hlo futa.. Kla mtu analengo na hakuna anaefwata mkumbo wala kundi bali dhamira yake mwenyewe. Kama hujui au unajua jarbu kusoma kwa makn maelezo ya clemmy yanaweza kukufungua zaid. Inakera unapotaka kumfanya mwanafunz wa chuo kkuu awe "askari" yani YES kwa kla ktu bla kuhoji!!!!??
 
Ndo tunaanza kuona athari za baadhi ya watu walafi kuhongwa vijisenti na kugawa rasilimali zetu kwa bei ya vitunguu. Tunashindwa kutatua matatizo ya msingi kabisa ya elimu ya vijana wetu tunabaki na frustrations za kuwapiga virungu na kuwatimua. Responsible leadership ilikufa kipindi cha mwalimu, hivi sasa ni selfish leadership. Sioni matumaini ya nchi inakoelekea, labda baadaye hali yaweza badilka. You never know
we should wake up hawa mafisadi hawawezi kuchezea majority of Tanzanian its our moment to fight for our right
 
Wanafunzi wa sasa waoga sana yani me ningekuwa mwanafunzi leo ningelipua makazi ya mkandara hapo,na kuna kipindi ticha flani hapo alikua ananizingua na nilipanga nilipue utawala sema tulienda nae sawa,hawa washenzi dawa yao ni kulipua yani mnashindwa kujioganaiz wanafunzi hata wa5 mkanunua guruneti na kulipua utawala? Kama mbwai mbwai tu hii nchi mbele haitotawalika biliv dat I'm tellin y'all buddiez
 
Back
Top Bottom