Mi nadhani Wa - TZ hasa wanaojiita wasomi wabadilike, ukitazama tangu mwanzo sababu iliyowafanya wagome haikuwa ya msingi, fedha hakuna, serikali imekopa huko duniani mpaka muda huu tunatukanwa hovyo hovyo, rejea matusi ya Ehud Barak wa Israel, David Cameron wa Uingereza na hata ripoti za karibuni zinzoonesha kwamba tunashika nafasi ya tatu kwa kusaidiwa Duniani ukiacha Iraq na Afganistani na bado wasomi hao hao waligoma na kuongezewa posho at their counterparts expenses ya kukosa masomo!! Sasa wasaidiweje hawa, hatuwezi kuwa na taasisi au nchi katika mawanda mapana ambayo viongozi wake hawana mamlaka. My take wale 43 waliofukuzwa mwanzo na ambao kesi zao bado zinaendelea ni sawa, hawa walioongoza ujinga eti mgomo wa amani na kufukuzwa jana ni sawa na wale waliosimamishwa wakibainika kufanya makosa wafukuzwe katika terms zile zile. Mi namshauri Makamu Mkuu wa chuo wa ukweli Prof. Mukandala kama kuna wengine watakaogoma fukuza kabisa baba! bakiza wanafunzi walio tayari kufanye UE tu ambao wanajua wamefata nini hapo chuoni.