1. Wazee wa jalalani walipewa Msaada na LIONS CLUB kufungiwa taa za solar kwenye barabara na mitaa main campus (bure) ukipita usiku hizo taa zimekufa karibu zote kumebaki Giza totoro. Mule ndani kwa sasa kumekua hatari sana.
Hivi Uongozi hapo wanaweza nini zaidi ya kununua Magari ya kifahari na viofisi vyao kama vyoo?
2. Chuo Kikuu kweli mnafikirisha aisee. Vyoo navyo mnasubiri Msaada toka Ulaya?
Tanzania na utunzwajwi wa Mali ya UMMA ni paka na panya! Pale Kigongo_Busisi lile Daraja halina hata miezi 6 pale toka lianze huduma ila karibia nusu ya Taa haziwaki sasa
Watu wetu wanawaza namna ya wao kujipatia kipato, kuhusu raslimali za uma hawana habari nazo.
Ziwepo, zisiwepo hawajali.
Hapo unawaongelea wasomi waliotukuka, hali inakuwaje kwenye maeneo mengine?