UDSM mbioni kuanzisha Udaktari

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kiko mbioni kuanzisha Shule Kuu ya Udaktari kwa ajili ya kozi za utabibu. Hiyo itakuwa ni hatua ya kurejesha Shule ya Udaktari baada ya Muhimbili kuwa Chuo Kikuu kamili. Katika kufikia lengo hilo, UDSM imetangaza nafasi 4 za kazi kwa Maprofesa, Maprofesa Washiriki, Wahadhiri Waandamizi na Wahadhiri wa Shule hiyo Kuu ya Udaktari.

Kuanzishwa huko kumebarikiwa na kikao cha Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lililoketi tarehe 11/8/2014. Tangazo la kazi lapatikana www.udsm.ac.tz

Hongera UDSM!
 
Ni Upuuzi Mtupu! sasa kwanini hizo fedha wasipeleka kuwekeza sehemu nyingine kama KCMC ,Mwanza (Bugando) au hata UDOM? ambako kuna vyuo vya Utabibu lkn bado ni vichanga? Dar si Tayari kuna Chuo kikuu cha Utabibu Muhimbili sasa kingine cha nini?
 
Kwanin muhimbili walijitenga?? Wataanzisha college ili ijitenge tena??
 
From MUCHS kama tawi la UD to MUHAS kama chuo kinachojitegemea. Vivyohivyo kwa uclas. Nini sababu ya kuviweka huru vyuo hivyo? Na kwanini kitengo kipya cha udaktari wa binadamu tena?

Tanzania na serikali ya CCM ni zaidi ya vioja!
 
Ndugu Kijakazi II, Napenda kukumbusha kusoma kwa makini maana mleata mada amesema shule kuu ya udaktari (Medical School). Hii itakua inafanya tafiti mbalimbali za kitabibu na kufundisha shahada za juu za mambo ya tiba siyo kama muhimbili au kwingineko unakosea. Pili huko KCMC na bugando siyo medical school na ki ukweli hamna medical school Tanzania.

Alafu pesa za kuanzisha kitu kama hicho si ya kutoka serikalini maana inahitaji pesa nyingi lazima itakua ni mradi tena wa ppp au kwa ushirikiano na vyuo vingine vya aina hiyo. Nilimsikia Makamu Mkuu wa UDSM akilisemea hilo na nilisoma salamu zake za mwaka mpya kwa wanajumuiya ya chuo hicho kuwa wanaanzisha medical school kwa patnership na Medical School fulani huko China na Los Angeles Medical School ambayo nadhani is the best in the world.

Nadhani cha msingi ni kuhoji ubora wa medical school hiyo na si kuchagiza hela zingeenda wapi sijui na mambo mengine kama hayo, hii si siasa wajameni.

Kila lakheri UDSM kwa kuona public need
 
nimeona kwenye guide book ya mwaka huu, ndo inaanza mwaka huu hyo coz? Manake sijawahi kuskia kabla udsm kuna md, na ni campus ipi, kwa mwenye ufahamu na hili.
 
Hawezi kuwa rahis hivyo ,hao waalim utawatoa wapi ,
 
nimeona kwenye guide book ya mwaka huu, ndo inaanza mwaka huu hyo coz? Manake sijawahi kuskia kabla udsm kuna md, na ni campus ipi, kwa mwenye ufahamu na hili.

Hakuna kitu kama hicho....rudia tena kuisoma hiyo guidebook uliyonayonayo......kama utaona hamna mabadiliko basi ni hiyo gbk ni fake.
 

Hiyo medical school na UDOM wanafungua kitu kama hicho!?
 

Hujui maana ya medical school, kaa kimya
 
Hujui maana ya medical school, kaa kimya

Nadhani tuache kubeza.Tunahtaji vıongozi wetu wawe wabunifu.Project km hyo wamekaa wataalam wakaiandikia.Hapo hakuna tatizo na ninadhanı hakuna hela ya serikali huko.Lazima tuwe na chuo au vyuo ambavyo ni complex japo hata viwili.Nawaomba wapanue na kuwekeza zaidi CoET.Bıgup UD.Wengne nao wachakalike, MUHAS wanashndwa kuandaa hata wahadhiri, hakuna walımu kabısa Muhas.Baadhi ya specialıties hazna hata prof.1.
 
Hakuna kitu kama hicho....rudia tena kuisoma hiyo guidebook uliyonayonayo......kama utaona hamna mabadiliko basi ni hiyo gbk ni fake.

niliyonayo nimeitoa tcu official website, labda kama yako original umeiona sehemu tofauti na hapo, page 285, university of dar es salaam(UDSM)-DOCTOR OF MEDICINE, Code yake ni UD080,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…