Kitila, wewe umeshawahi kujinyima kipande chako cha mkate na kumpa unayedhani kuwa ana njaa kisha akautia mchanga? Kama uliwahi kukutwa na hayo ulijisikiaje?
Nina uchungu sana, mjukuu wangu yupo mwaka wa tatu, mitihani kanambia wataanza wiki mbili zijazo, kisha akifukuzwa inakuwaje? Nihangaike tena?
Mjukuu wangu huyu nimehangaika naye tangu vidudu, nimemsomesha, kesho kutwa naiona digrii hile, halafu alete ujinga?
Kuna rafiki yake Aggy kanipigia simu sasa hivi anasema huko polisi wanarusha mabomu na kuwa watu wameumia. Na huyu aggy hajui alipo. Hapa nilipo tumbo linawaka moto. Aggy mjukuu wangu hana simu.