UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

Gembe unajiabisha!

Rudi chuoni pale kivukoni maana naona hujakomaa kwenye propaganda za makamba
Na wewe ndio hukosea zaidi, kila kitu kiendacho kinyume na lengo la masikio yako basi ni cha CCM...! Namna gani mdada!
 
Asante Kitila,

Hili ndilo mimi napigania hapa. Hawa wanafunzi wananyimwa haki yao ya kuchagua viongozi wao kwa mujibu wa katiba zao. Wakigoma au kufanya shinikizo, wanakamatwa, wanapigwa kwa excessive force na mengine mengi.

Tunategemea kujenga taifa la namna gani?

Wanafunzi wa UD, poleni sana kwa mnayopata lakini mnachopigania si bure. Watanzania wote wangekuwa na moyo kama huu basi leo hii tusingekuwa na Buzwagi, Richmonduli, vijisenti, kula nyasi, na mengine mengi.
 
Hakuna uhalifu wowote waliofanya zaidi ya kudai haki zao. Msingi wa mgomo huu ni uongozi wa chuo kuingilia demokrasia ya wanafunzi wasomi kuchagua viongozi wao.

Huu ni uzembe na upuuuzi wa hali ya juu sana!
 
Mkuu Ben,

Hakuna ugomvi wowote kati yangu na mama. Mama ni mmoja wa memba wanaoheshimika sana hapa forum. Imekuwa tu yeye yuko upande wa kina Mkandala kwenye hii case na mimi niko upande wa wanafunzi.
 
It is not that simple Mamkwe. Binadamu haishi kwa mkate tu!
Kitila, wewe umeshawahi kujinyima kipande chako cha mkate na kumpa unayedhani kuwa ana njaa kisha akautia mchanga? Kama uliwahi kukutwa na hayo ulijisikiaje?

Nina uchungu sana, mjukuu wangu yupo mwaka wa tatu, mitihani kanambia wataanza wiki mbili zijazo, kisha akifukuzwa inakuwaje? Nihangaike tena?

Mjukuu wangu huyu nimehangaika naye tangu vidudu, nimemsomesha, kesho kutwa naiona digrii hile, halafu alete ujinga?

Kuna rafiki yake Aggy kanipigia simu sasa hivi anasema huko polisi wanarusha mabomu na kuwa watu wameumia. Na huyu aggy hajui alipo. Hapa nilipo tumbo linawaka moto. Aggy mjukuu wangu hana simu.
 
Hakuna uhalifu wowote waliofanya zaidi ya kudai haki zao. Msingi wa mgomo huu ni uongozi wa chuo kuingilia demokrasia ya wanafunzi wasomi kuchagua viongozi wao.

Huu ni uzembe na upuuuzi wa hali ya juu sana!

Na kibaya zaidi wasomi wazima ma (prof) kujifanya mdebwedo
 
Mlimani pamechafuka sana na huo ni ukweli ila kitendo hiki kitakiweka chuo kwenye mazingira ya kufungwa.

Vijana wa uhandisi wameamua kujiunga rasmi kwenye maandamano ya leo na hapo ndio polisi waliitwa kuja chuoni ila bado wanajipanga kama nilivyosema jana .
 
Migomo mingi sana ya mlimani inafanikiwa
Kama kuna migomo mingi iliyokwisha fanikiwa ni vema wakarudia kwenye makablasha ya migomo hiyo ili kuweza kupata mbinu zilizo tumia. Kwani hadi sasa JF imeshindwa kutoa njia ya kuweza kufanikisha mgomo wao.

Wanafunzi wa UD, poleni sana kwa mnayopata lakini mnachopigania si bure. Watanzania wote wangekuwa na moyo kama huu basi leo hii tusingekuwa na Buzwagi, Richmonduli, vijisenti, kula nyasi, na mengine mengi.

Wanamlimani kwa kauli yako ya pale juu wamekuwa wakishinda migomo mingi, na huu sio wa kwanza, hivyo kuna idadi kubwa kabisa ya waliopitia mlimani ambao wapo mitaani na bado kuna skandari nyingi tu...!
 
Hakuna uhalifu wowote waliofanya zaidi ya kudai haki zao. Msingi wa mgomo huu ni uongozi wa chuo kuingilia demokrasia ya wanafunzi wasomi kuchagua viongozi wao.

Huu ni uzembe na upuuuzi wa hali ya juu sana!

Hilo la uongozi wa chuo nalielewa, au kwa vile ni Mtatiro yumo basi nisihoji chochote. Sitaki malumbano period!
 
Mkuu nyangumi,

Hawa vijana wamekuwa wanatoa matamko mengi tu hapa kuhusu hali ya ufisadi inayoendelea Tanzania. Huyu kijana Mtatiro ni very active kwenye masuala ya nchi na serikali ya ccm haimpendi na hata waziri wa elimu ya juu ameonyesha hilo.

Ni very wrong kusema kuwa hawa ni mabishoo na kuwa hawajali hali ya nchi wakati ukweli umeonyesha kuwa ni vijana wanajali hali ya nchi yao hata pamoja na mazingira magumu wanayosomea.
 
Utawala unawaogopa sana maengineer, unajua wakiingia hao jamaa moto wao si wa kipole pole.
 
Hakuna uhalifu wowote waliofanya zaidi ya kudai haki zao. Msingi wa mgomo huu ni uongozi wa chuo kuingilia demokrasia ya wanafunzi wasomi kuchagua viongozi wao.

Huu ni uzembe na upuuuzi wa hali ya juu sana!

Nakubaliana na wewe, dada! Tatizo ni kwamba UDSM kwa miaka mingi imekuwa politicized na itaendelea kuwa hivyo kutokana na kuwa:
1. Wanafunzi na vijana wasomi kwa kawaida hupenda sana masuala ya siasa na wanajaribu ku-apply wanayoyafunza darasani including democracy
2. CCMi litambua mapema kuwa chanzo cha dissent duniani ni kwa vijana hususan wanavyuo, kwa hiyo imekuwa ikifanya jitihada makusudi kuhakikisha kuwa wanaingilia uongozi wa wanafunzi. Ndiyo maana kila baada ya miaka kadhaa wanafunzi hutimuliwa (hata akina Sitta walitimuliwa!)

Lakini hii ya leo kuleta FFU naona ni TOO MUCH! Hao wanafunzi walikuwa wanatishia vipi amani? Labda tuendelee kupata habari.
 
Mjukuu wako akijiangalia peke yake atakuwa mbinafsi wa hali ya juu. Kumbuka aliyevujisha siri za serikali hapa JF naye alikuwa anafikiria kuwa anaweza kukamatwa na akawekwa ndani na familia yake ikapata shida.

But you know what, alivujisha mikataba na siri za serikali anyway kwa sababu kwake huyo, maisha ya watanzania wote ni muhimu zaidi kuliko yeye binaafsi.

Angekuwa mbinafsi, angekaa kimya ili kulinda kibarua chake. Unajua kuwa kuna watu wanafuatiliwa benki ya posta kwa vile wamevujisha siri za ufisadi huko? Hawa wangekuwa na mawazo kama yako wangekaa kimyaaaaaaaa
 
Kuna mtu kanitumia email akini-update na hali ilivyo chuo; inaonekana hali sio shwari. Ni kama vita. I am surprised and shocked maana sijasikia cha kutisha walichofanya hawa wanafunzi hadi waletewe polisi wenye masilaha yote haya. It looks lile the leadership failure in our country is right across the board! Herebelow I share with you some few phrases from the email I received.

Kwa hiyo ile kitu inaitwa Kunji au FoE spirit bado kipo??
 
Hilo la uongozi wa chuo nalielewa, au kwa vile ni Mtatiro yumo basi nisihoji chochote. Sitaki malumbano period!

Hakuna malumbano mama, unaweza kuhoji chochote unachopenda na ukapata majibu kama kawa ya JF. Ukipata majibu yako basi usiyachukulie kama malumbano. Okay?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…