Wana JF,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka hivi (ninanukuu):
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au ashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
Tukiangalia mtazamo (au reaction) ya dola, kwa kuwatumia askari polisi 'kuwatuliza' na au kuwanyamazisha wanafunzi pale ambapo walikuwa wamekusanyika (mara nyingi kwa amani), fujo na vurugu huanzia pale ambapo polisi wanapowalazimisha wanafunzi hao kutawanyika, wanapokataa kutii amri hiyo, humwagiwa tindikali, maji yanayowasha, mabomu ya machoni, n.k., mambo ambayo yanawafanya wa-react kutokana na sababu za kisaikolojia (self defence).
You will always defend yourself when attacked!
Kama serikali ingekuwa inakubali majadiliano na kuwapa wananchi uhuru wa kupinga (right of peaceful assembly, vis-a-vis public procession), basi, hakungekuwapo na matukio ya vurungu, uvunjwaji wa sheria, n.k.
Nani alaumiwe? Aliyedai haki yake kwa kuandamana au aliyekwenda kumnyamazisha asiidai haki yake, kwa kumpiga virungu, kumwagia maji ya upupu na mabomu ya machozi?
Jambo hili linanikumbusha mwaka 1995, wakati Serikali, Mkoani Kilimanjaro, iliposema kwamba isingewamwagia watu mabomu ya machozi wakati walipokwenda kumpokea aliyekuwa mgombea urais wakati huo, kupitia chama cha kisiasa cha NCCR-Mageuzi, Augustine Lyatonga Mrema.
Watu hao walikusanyika pembezoni mwa barabara (nilikuwa mmoja wa waandishi wa habari waandamizi tuliokuwa na Mrema wakati wa ziara yake, tukiripoti matukio mbali mbali...), wakisubiri kumlaki Mrema, kwa amani. Magari ya FFU na askari wakapita barabarani wakitupa mabomu ya machozi, watu walikimbia nyumbani kunawa nyuso zao, na kurudi tena barabarani! Ilikuwa aibu na kichekesho cha mwaka!
Lakini ya UDSM ni mengine... wako wanaotoa lawama, na wako wanaowaunga mkono. Zote hizo ni hoja, ni maoni, kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake... Ibara ya 18 (1) na (2) ya Katiba!
Someni katiba muielewe waungwana!
./Mwana wa Haki