Heshima kwako mkuu,
Unajua wewe wakati mwimgine nakufananisha na wale vibaraka wa Makaburu enzi zile wasauzi wanapigania uhuru wao kutoka kwa makaburu wale waafrika ndio walikua mstari wa mbele kuwakatisha wenzao tamaa.
Hapo UDSM kuna uonevu wa kutisha na sasa kama ni mabadiliko ya nguvu lazima yaanzie hapo.
Vijana jengeni hoja za nguvu ambazo hata mkiziweka katika jukwaa la kimataifa zitakubalika hata ikiwa worse kufikia hatua za kuandikwa na vyombo vya habari vya kimataifa zionekane logic za kweli.
Kisha watengeni wale ambao wana uchungu wa kudai haki na wale waoga wachache ambo inawezekana uoga wao unatokana na kutokuelewa umuhimu wa mnachofanya.Kisha hilo kundi la ambao wanaogopa kugoma mtafute kijikamati kidogo cha watu wenye ushawishi mkubwa na wanaoweza kusikilizwa na makundi yote ya wanafunzi halafu wawashawishi kwa kukaa upande wao kwanza ili wafanane.Wawaeleze kwanza hasara za kugoma na kisha waombe sapoti ya hilo kundi kwa wale walio katika ari ya kugoma.Tarehe ya kuanza mgomo itangazwe rasmi na taarifa zipelekwe kwenye vyombo vya habari ikiambatana na maandamano ya nguvu lakini ya amani na yenye kila dalili ya kuwa hakuna kulala mpaka kieleweke.Mkishashinda hapa,mtakua mmekomaa kiasi ambacho mtaweza kushinikiza kufanyika kwa mambo makubwa ya kitaifa.
Msiogope polisi hata kidogo.Hata hivyo kama mtu hujui haki yako au kama hujui kwa nini unagoma ni bora usigome.
Tumieni Nguvu ya Umma