Parapanda Litalia parapanda - Hii ndio nyimbo iliyokuwa inaimbwa na wanafunzi waliokuwa wanaandamana kutokea UDASA wakapita Hall 6 mpaka kuelekea utawala , watu waliokuwa upande wa hall 6 na 7 walikuwa wanasikia vilio vya watu tu huko juu utawala , baadhi ya wanafunzi walikuwa nyumbani mwao wengine katika korido , wengine njiani wakiwashangaa wenzao , wale waliokuwa wanaandamana wengine walishika matawi ya mili , wengine vitambaa na hata wengine walibeba maji maji haya ni ya kujiandaa kama polisi wakivurumusha mabomu ya machozi tena waweze kujiosha nyuso zao .
Mbele kabisa kulikuwa na wanafunzi kama 6 hivi wote walikuwa wamebeba bango moja lilioandikwa kwa mkaa inaonyesha wanafunzi hawa hawakujiandaa ndio maana wanakuwa na bango ambali halisomeki vizuri wala nini , pamoja na wanafunzi kuandamana hivi sikuona vyombo vyovyote vya habari pembeni yao au nyuma yao kuweza kuhoji au kudadisi ni nini haswa wanafunzi wanachotaka .
Pia wapiga picha za televisheni hawakuwa pamoja na wanafunzi hawa waandishi wengi walikaa upande wa askari wa kuzuia fujo upande ule wa utawala , wengine walikuwa hall 7 wakihoji wanafunzi ambao hawajaandamana , sijaelewa kwanini haswa waaandishi hawataka kuwahoji wale wanaoandamana nao waongee chao , tatizo lengine ni kwamba hawa wanaoandamana hawana msemaji wao kwahiyo inakuwa ngumu sana kuweza kufuatilia au kukaa meza moja na uongozi wa chuo
Binafsi nilijaribu kumtoa mwanafunzi mmoja niongee nae kujua nini kinaendelea yeye akabaki kusema tu hatumataki mkandara , ukiuliza kwanini hajui jibu kwa nini , lakini pia kuna tatizo lingine kubwa baadhi ya wanafunzi wanasema wengi wanaoandamana wamekuwa na matatizo na chuo kwa muda mrefu wengi wao hawajamaliza kulipa adda zao wanazodaiwa na chuo kwahiyo nao wanajiingiza katika mgogoro huu .
Mpaka namaliza kuandika ukurasa huu hali ya chuo kwa sasa imetulia wanafunzi wanangoja kusikia chochote kutoka kwa uongozi wa chuo watasema nini waende nyumbani au wafanye nini , kuhusu mauaji yaliyotokea jana hapa chuoni , ni kwamba bomu hilo lilikuwa ni la machozi na lilipigwa katika mghahawa wakati wanafunzi wanapata mlo na kufanya mambo mengine ya kiafya
Hakuna upande wowote unaosema kwanini polisi waliamua kurusha bomu la machozi ndani ya kafteria au mule ndani kulikuwa na nini haswa lakini bomu hilo lilianguka karibu na mama mja mzito huyu mama akakosa kupumua vizuri na ndipo mauti yake yalipomkuta , maajabu ilikuwa hata watu wa msaada wa kwanza hawakuwa pale wanafunzi wachache walijaribu kumuokoa ikashindikana kweli kazi ipo humu ndani .
Na mwisho kabisa , maandamano haya yanayoendelea katika eneo la chuo ni batili hayajarihusiwa na mtu wowote yule , na hata kama yangeruhusiwa kuna sehemu zake za kupitia katika maandamano yoyote ili kuepusha fujo au uvunjaji wa amani kwa njia yoyote ile lakini maandamano ya wanafunzi haya ni tofauti kabisa wanapita katika mabweni ya wanafunzi wenzao ambao hawajagoma , wanatishia kupiga baadhi ya watu na wamesababisha hasara kwa baadhi ya biashara ndani ya eneo la chuo hayo ni makosa je watakuwa tayari kulipa hasara hii siku wakitakiwa kufanya hivyo ?
Hii nyingine sijui ni tatizo la mawasiliano au ni hujuma tu inayoendelea kutokana na maandamano haya huduma za mawasiliano ndani ya chuo zimekuwa za taratibu au hazipatikani kabisa mfano wale wanaouza kadi za simu hawauzi ingawa wako katika biashara zao huduma ya internet iko slow sana au kuna kipindi ilikatwa kabisa watu walishindwa kuwasiliana na ndugu na jamaa zao ndio maana usishangae kwanini habari hizi ziko kimya sana watu hawachangii katika blogu na forum zingine ni kuhusu uslow down wa huduma hii