The lariat
JF-Expert Member
- May 16, 2025
- 1,351
- 1,928
Jukumu la makazi/malazi lipo juu ya mwanachuo, na sio serikali au chuo, that's why wanapewa hela ya mkopo kwa wanaohitaji. Ujenzi wa hostels ni upendeleo tu, si lazima.Kama mradi huu ni eneo la Chuo wasisahau pia na kujenga Hostels za kutosha ili wanafunzi waweze kukaa karibu na Chuo (after all hao wanafunzi ndio first Product kulingana na objectives zao); Nawakumbusha tu wasijejikuta Primary Objective inakuwa Secondary and Vice Versa...;
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chasaini Mkataba Mkubwa kwa Mradi wa Kituo cha Biashara cha Hill Park
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investments kimesaini rasmi mkataba wa TZS bilioni 8.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ndoto wa Hill Park Business Complex.
Mradi huu utakaochukua eneo la mita za mraba 12,498.5 utajumuisha maeneo ya biashara, migahawa, benki, huduma za urembo, huduma za ukarimu, maeneo ya kuchezea watoto, na huduma nyingine nyingi—zote zikilenga kuhuisha maisha ya chuo na kuhudumia jamii kwa ujumla.
Hii ni hatua ya kishujaa kuelekea uzoefu wa kisasa, wenye mvuto, na unaojitegemea kifedha kwa wanafunzi na jamii ya chuo.
Waanzishe na miradi ya kufyatua tofaliNchi ya wachuuzi kila kona ni frames tu. Watu bunafsi, taasisi hadi vyombo vya ulinzi na usalama wote wanawaza uchuuzi tu.
Na hao ma researchers wa kuweza kukimbizana na ulimwengu unaobadilika kwa kasi ndiyo kama nyie, au tutaagiza kutoka nje?Sema tunajua kutupa pesa, haya ma-eneo ya kula bata, business parks n.k yamekua mengi sana mjini.Hapo tu jirani Mlimani City ipo inajitosheleza, uswahili kila kona wachina, wahindi wamemwaga the same investments.
Watu indivifually kila mtu anajitutumua, hapo ubungo kuna wachina wameishafanya kufuru..sasa hawa nao wanajenga la nini??
Hawawezi kuwekeza kwenye research institution ambayo iko well funded ili tukimbizane na ulimwengu unaobadilika kwa kasi???
Research center unajenga kwa hela ipi?Badala ya kujenga research center wao wanajenga "frames'?
Nawaza tu hivi mwendokasi imewashinda kabisa watu weusi kuwekeza ?
Hiki chuo bana badala kianzishe hata research centre na lab za kimataifa kinadeal na mambo ya biashara tu.
Jukumu la makazi/malazi lipo juu ya mwanachuo, na sio serikali au chuo, that's why wanapewa hela ya mkopo kwa wanaohitaji. Ujenzi wa hostels ni upendeleo tu, si lazima.
Hilo eneo kubwa namna hiyo ,liko upande Gani WA UDSM au wanahamisha wananchi
Michina lazima ipo hapo nyuma.
Hawa baswahili wanawaza uji tu kichwani na hiyo misuti yao.
Hao watumishi wenyewe watanufaika na nini maana maisha yao ni Mungu nisaidieChuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investments kimesaini rasmi mkataba wa TZS bilioni 8.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ndoto wa Hill Park Business Complex.
Chuo cha UDSM csmpus ya DSM hawana eneo la kufanya hayo mambo yote wanayotaka na ambayo hayana tija yoyote.Na mimi nilitaka niulize swali hilohilo
Imetosha sasa chuo kinahitaji eneo la parks na mandhari ya kupendeza ya miti na nyasi
Sio mijengo kila mahali utafikiri Kariakoo. Baadhi ya Prof na Dr. hapo si wamesoma vyuo vya mbele
Wamesahau jinsi mandhari ya vyuo vya wenzetu inavypendeza na uoto saafi hewa ya kutosha na sehemu za kupumzika
Sio mijengo jengo kila kona. Majengo yaongezwe yanayohusiana na kuboresha taaluma tu
Ila Mlimani City iko hai, hii inakaaje kibiashara, naona kutakuwa na sehemu za mabenki, na bank zote ziko Mlimani City, watahama?Wazo hili lilikuwepo toka miaka ya 2004 halikutekelezwa ipasavyo ikazaliwa Mlimani City.