UDSM yaingia mkataba kujenga kituo kikubwa cha biashara zaidi ya Mlimani City

UDSM yaingia mkataba kujenga kituo kikubwa cha biashara zaidi ya Mlimani City

FYI ili eneo la Hillpark lipo muda mrefu ni opposite na Shule Kuu ya Biashara ,ni la zamani na limechoka sana hvo wameingia ubia kulitengeneza na kuwa ula kisasa , kama mnavojua UDSM nzima hamna recreation centre yoyote ukiachana na hill park ambayo ishakuwa mahame , so msikurupuke kuandika bila kufanya tafiti
Unajua maana ya utafiti?
 
Jukumu la makazi/malazi lipo juu ya mwanachuo, na sio serikali au chuo, that's why wanapewa hela ya mkopo kwa wanaohitaji. Ujenzi wa hostels ni upendeleo tu, si lazima.
Kwahio unajenga Chuo Huweki Hostels za kutosha watu binafsi ambao wapo pale for profit wanachukua real estate ya kutosha sababu demand ni kubwa kuliko supply bei inapanda au wengine kuishi sehemu za mbali sababu zote za karibu zimejaa... !!!!

Kwahio huo Mkopo utasustain bei ya Market ambayo kutokana na demand ipo juu kuliko uhalisia ?

Kwamba provision ya Hostel kwa wanachuo ni upendeleo na sio lazima ?!!!!
 
Udsm ina maeneo mengi sana. Sehemu za kujenga hostel hazijawi kuisha
Zinatosha ? Wanazijenga ? Au hicho sio kipaumbele ? Kipindi hao wanaoingia mikataba sasa wanasoma capacity yao ilikuwa ni equivalent na Makazi au na wao nafasi zilikuwa hazitoshi ? Kama zilikuwa zinatosha na sasa hivi hazitoshi tambua kwamba kuna sehemu waliteleza
 
Napinga huo mradi. Utaathiri makazi ya ngedere, kenge, nyoka, ndege na bioanuai zingine. Tuache ufilisti.
 
Jukumu la UDSM ni kutoa elimu na research sio kuingia kwenye mikataba mibovu.
Ajabu ni kwsmba siku hizi utamkuta msomi mwenye masters degree ni chawa.
Enzi za professor Mmari hakuna ambaye angemvaa prof. Kuingia keenye mikataba ya michongo.
Eti salon za urembo.
Hili la Mlimani City, Prof. M. Luhanga alilipinga lakini akashindwa maana wakubwa walimkalia kooni.
 
Kwahio huo Mkopo utasustain bei ya Market ambayo kutokana na demand ipo juu kuliko uhalisia ?
Kwamba provision ya Hostel kwa wanachuo ni upendeleo na sio lazima ?!!!!
Hostel ni optional kwa Taasisi, kama mkopo hautoshi hilo ni jambo lingine.
 
Hostel ni optional kwa Taasisi, kama mkopo hautoshi hilo ni jambo lingine.
Ndio maana nakwambia Karne hii watu vipaumbele vimekuwa Vice Versa no wonder tunazidi kupotea...

Nini kazi ya Chuo katika Jamii (Je ni kuhakikisha inatengeneza faida as much as possible au kuhakikisha bright minds wanaweza kuongeza maarifa na kufanya research ambazo zinasaidia taifa kutoka na requirements za wakati husika na Gap of what is needed)

Kama issue ya maana ni kukusanya bright minds za nchi nzima ili ziweze kutoa matunda ya kifikra na ufahamu watu hao lazima uwapatie basic needs ambapo ni kuhakikisha pamoja na malazi ni affordable...

Bila kuwa na hostels za kutosha ni kwamba una create demand na kama mtu anayekidhi hizo demands atakuwa private basi tegemea bei zitakuwa juu kuliko uhalisia (sababu mtu binafsi yeye hayupo kwa ajili ya huduma yupo to get as maximum profit as possible) Ndio maana nilivyoona hata Karulila analeta story za PPPs za Mabweni nikasema huu ni mwendeleozo wa ku lose the plot...

Sijasema wasifanye Biashara yoyote wanaweza kufanya lolote wanalotaka kufanya lakini katika core requirements ni kuhakikisha mwanafunzi anapatiwa kwanza requirements zote na Hostel ni moja ya requirements hizo

Hata ukiwapa watu mkopo wa Trillion sita kama karibia na vyuo hakuna Supply ya kutosha na Demand ni kubwa basi vyumba vitapanda bei maradufu (watu hawana option) ndio maana sehemu kama Dar Rent sio sawa na huko Vijijini
 
Nawaza tu hivi mwendokasi imewashinda kabisa watu weusi kuwekeza ?
Mwendokasi ya bongo haijawahi kulipa na haitalipa kamwe. Ndio maana kila anayetaka kuwekeza anatanguliza capacity charge ili kodi yako ndio imlipe faida. Tulijua machungu ya capacity charge ya Richmond kwa Bunge la Standard and Speed, sasa kwa Bunge hili la Chawa sijui kama tutakuja kujua kinachoendelea.
 
Nauli ya 700 inaweza kulipa basi la milion 400 na mishahara ya kuoperate huduma?

Ndio. Mbona dala dala zinachaji nauli hizo hizo na eicher na tata zinauzwa hela nyingi huku zinabeba abiria wachache tu sawa na robo ya abiria wanaobebwa kwenye bus moja la mwendokasi
 
Hiki chuo bana badala kianzishe hata research centre na lab za kimataifa kinadeal na mambo ya biashara tu.
Taifa matopeni imagine hata maprofessor wengi uwekezaji wao ni Lodge na viduka vya pombe wanavipamba kwa jina la kingereza eti 'Liquor Store'
 
Back
Top Bottom