UDSM yaingia mkataba kujenga kituo kikubwa cha biashara zaidi ya Mlimani City

Ila Mlimani City iko hai, hii inakaaje kibiashara, naona kutakuwa na sehemu za mabenki, za bank zote ziko Mlimani, watahama?
Akikujibu ni tag, maana hata sehemu za kuchezea watoto zipo, hata salun zipo. Sina hakika kama ni habari ya sasa hivi hii.
 
Badala wajenge research facilities, makumbusho na viwanja vya michezo wao wanajenga fremu za biashara!
Tena kama pale udsm na hizi afcon inakuja wange tandinka viwanja vya mpira kama 7 hivi na research centre kwa ajili ya watu wanaosomea sport science....hiyo 2027 wanafunzinzi wangwpata kufanya field na research hapo hapo chuo huku wanaingkza hela nyingi tuu.
 
Hiki chuo bana badala kianzishe hata research centre na lab za kimataifa kinadeal na mambo ya biashara tu.
Upigaji. Hawana lolote na hapa ni watu wanatafuta ulaji. Kumbuka chini ya ma-ushungi, kila kitu kinapigwa bei na kugeuzwa sehemu za biashara.
 
Akili za Mwafrika hata akiwa msomi kuzielewa na ngumu sana, yani chuo kikuu miradi wanayofikiria ni fremu za maduka ya biashara! 🤣 Msiba huu.
 
Akili za Mwafrika hata akiwa msomi kuzielewa na ngumu sana, yani chuo kikuu miradi wanayofikiria ni fremu za maduka ya biashara! 🤣 Msiba huu.
Mwafrica ni nyani aliye changamka changamka
 
Pili wana eneo huko bahari beach wameliacha vibaka wanakaa, lile ndo wangeendeleza linafaa kwa biashara kama hizo Leo wanakimbilia kujenga flemu za maduka na kuleta makelele chuoni.
 
Ile mandhari,nature yote inapotea hapo udsm .......

Ova
 

Nilifungua kwa haraka nikitaraji kuona wanajenga kituo kikubwa cha UTAFITI (Research center)
kama vyuo vikubwa duniani

Binafsi nafikiri ipo haja ya kuanza tena kuviangalia hivi vyuo vyetu hasa vya serikali
Utakuta Course nyingi zilizokuwa zinatolewa SUA kimkakati kwa sababu ya mazingira na kuwa na Eneo kubwa na UDSM wame zianzisha tena kwenye mazingira ya kuunga unga ili tu wapate wanafunzi
Inamaana kuna namna tunahamia kwenye biashara kuliko Elimu...
 
FYI ili eneo la Hillpark lipo muda mrefu ni opposite na Shule Kuu ya Biashara ,ni la zamani na limechoka sana hvo wameingia ubia kulitengeneza na kuwa la kisasa , kama mnavojua UDSM nzima hamna recreation centre yoyote ukiachana na hill park ambayo ishakuwa mahame , so msikurupuke kuandika bila kufanya tafiti
 
Chagueni Wabia wazuri. Hao watakuja kuwaharibia. Miradi wanayojenga siyo miradi ya viwango.
 
Ndio hivo sasa hayana akili wala vision.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…