UDSM Yapandisha Kodi ya Malazi ya Wanafunzi na Ada za Huduma za Chuo Kuanzia Mwaka wa Masomo 2026/2027

UDSM Yapandisha Kodi ya Malazi ya Wanafunzi na Ada za Huduma za Chuo Kuanzia Mwaka wa Masomo 2026/2027

tucker carlson

Senior Member
Joined
Oct 5, 2025
Posts
182
Reaction score
759
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika Mkutano wake wa 301 limeidhinisha mabadiliko ya viwango vya kodi ya malazi katika mabweni na hosteli za wanafunzi, pamoja na gharama za huduma za moja kwa moja za chuo (Direct University Costs) kuanzia mwaka wa masomo wa 2026/2027.

Sababu za Kuongezeka kwa Kodi ya Malazi​

Kulingana na taarifa iliyotolewa na chuo hicho, mapitio ya kodi ya malazi yalifanyika mara ya mwisho miaka 13 iliyopita, jambo lililofanya viwango vya zamani kutolingana na gharama halisi za uendeshaji na matengenezo kutokana na mfumuko wa bei.

Imeelezwa kuwa gharama za sasa za uendeshaji wa mabweni hayo ni takribani shilingi bilioni 5.4 kwa mwaka, wakati makusanyo ya kodi kwa mwaka ni shilingi bilioni 2.25 pekee, hivyo kuwepo kwa haja ya kuboresha miundombinu, kununua samani na kuboresha utoaji wa huduma za malazi kwa wanafunzi.

Viwango Vipya vya Kodi ya Malazi (Shahada ya Awali)​

Wanafunzi wa Shahada ya Awali (Undergraduate) wa Kitanzania watalipa viwango vifuatavyo vya malazi:

  • Mabweni Na. 1–7, Jaji Julie Manning, Hosteli ya Magufuli, CoICT, Kunduchi na MCHAS: Shilingi 1,300 kwa siku (TZS 154,700 kwa semesta).
  • Hosteli za Mabibo na Mazizini: Shilingi 1,000 kwa siku (TZS 119,000 kwa semesta).
  • Mabweni ya Kagera, Ngongo, Ruangwa na Buyu: Shilingi 2,000 kwa siku (TZS 238,000 kwa semesta)
darusomlimani_1791017858_3999665589057699385_8472242936.jpg


darusomlimani_1791017858_3999665589057639555_8472242936.jpg
darusomlimani_1791017858_3999665589955193120_8472242936.jpg
 
Sio mbaya. Mfano, SAUT hii hapa, karibia 340k.
1550.png
 
Wafanye double ya hiyo kabisa!
 
Back
Top Bottom