Nilisoma UDSM Bsc In Umeme, wakati nikiwa high school nilitamani sana kufika chuo kikuu na nilikuwa na mategemeo makubwa ambapo nilipofika mambo yalikuwa tofauti kabisaaaa. Four years later, nimemaliza UDSM nikapata kazi mkoa na baadae nikaamua kutafuta nafasi nikasome zaidi!! Cha ajabu naongea kile ninachokiona, yale mambo nilikuwa nategemea kuyaona nilipokuwa UDSM sasa ndo nayaona, the university train student how to think critically siyo kukimbia kimbia tu.
Back to UDSM, Kuna shida nyingi sana ambazo admnistration hawataki kushughulika!! Ili uwafanye watu wasome, wafundishe, wazalishe, wafikirie critically basi huna budi kuboresha mazingira ya utolewaji wa taaluma.
1)UDSM hilo ni kinyume chake, utakuta vyoo vinanuka, havina maji, ofisini vumbi hadi utando, pazia za ofisini zina miaka 5 - 10 bila kubadilishwa na huweza kukaa hata mwaka mzima bila kufuliwa - Source: Mimi mwenyewe nimejionea et al.
2) UDSM haiwajali wafanya kazi wake, Prof and Dr. in some departments, hawa watu wanahitaji ofisi pamoja na Laboratory kwa ajili ya kutrain graduates students, kinyume chake wameachwa hivyo hivyo na kinachofanyika ni kikundi cha watu wachache wanaweza kujianzishia kamradi ka course fulani ya graduate ili kuendeleza knowldge zao huku wakiwa busy kufundisha vyuo vingine. - Source: Some staff from UDSM.
3) Hostels na Nyuma za walimu: Ukisikia UDSM na vyuo vingine vya Tanzania, its cracking!! watu wanabebana,mijitu ya miaka 22 - 40 wanalaa kwenye 4 by 4 watu wawili kweli, kwenye chumba cha kulala watu 2 wanalala hadi 5, its too bad. Huwezi kuconcetrate na kusoma, utasoma darasani mchana!! sometimes unahitaji kupumzika, ukienda room unakutana na room mate wamelala au wanasoma, au ratiba zinatofautiana, hapo elimu haiendi. Very frustrating university. Walimu ndo usiseme.
UDSM have to change, tena wasingeacha hiyo tabia ya kutoajiri walimu, chuo kilikuwa kinapotea kabisa kwenye ramani.