Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), William Kabogo, amesema hakuna taarifa zozote za serikali zilizopotea au kuibwa na wadukuzi baada ya tovuti kadhaa za serikali kuvamiwa mapema Jumatatu.
Miongoni mwa tovuti zilizodukuliwa ni ya Ikulu pamoja na zile za Wizara za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Afya, Elimu, Kazi, Mambo ya Ndani, na Mazingira.