SoC02 Uduni wa taarifa(Data), ni chanzo cha huduma mbovu za afya

SoC02 Uduni wa taarifa(Data), ni chanzo cha huduma mbovu za afya

Stories of Change - 2022 Competition

MulegiJr

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
125
Reaction score
88
Ubora Wa Taarifa (Data Quality), Ni mnyororo wa Taarifa sahihi za mtu, kitu au huduma Fulani katokana na mahitaji au Mazingira ya Umuhimu wa taarifa hiyo.

Huduma Bora ya Afya, Ni Mnyororo sahihi wa upatikanaji wa taarifa za kiafya kutoka kwa Watoa huduma, Kituo Cha Afya au kitengo maalumu kwa ajili ya kutoa taarifa katoka eneo maalumu ambazo zitapelekea utatuzi wa changamoto zinazozuia kwa namna moja au ingine upatikanaji wa huduma Bora za kimatibabu au miundombinu ya kutolea Huduma sahihi na kwa Wakati.

UTANGULIZI
Katika kiwanda Cha Huduma ya Afya Ni eneo ambalo linatoa taarifa duni, kuliko eneo lolote lile kwa sababu ya kukosa mfumo sahihi wa uhalili na ulindaji wa taarifa kutoka kwenye Vyanzo vyake, Kama vile taarifa Duni kuhusu Lishe, kuhusu ugonjwa wa uviko na zoezi la uchanjaji wake, Taarifa kuhusu chanjo za kawaida za watoto hasa hasa upande wa Polio na Pia Eneo la Ufatiliaji Magonjwa ya Mlipuko ( Disease Surveillance) , taarifa hizi Ni taarifa muhimu zinazohitajika na Wizara na Wadau kuweza kusaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa Ubora wa Huduma na zinazoweza chochea au kuwavutia Wadau kuleta mipango sahihi juu ya changamoto zilizopo katika Sekta ya Afya.

Mara ya Mwisho katibu mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Makubi alitoa Rai kwa Vituo vya Huduma ya Afya kuhakikisha wanatoa Huduma Bora Kama Msingi wa kufikia mahitaji ya Utoaji Huduma Iliyobora kwa Watanzania.

Mifumo ya Ukusanyaji Taarifa na Vyanzo vyake umekuwa Ni mfumo unaopitia marekebisho mengi ya kisasa, Lakini kurekebisha ya kimfumo yamemsahau Mtoa taarifa ngazi za chini kuwa ndie chanzo halisi ya Taarifa Duni na nguvu kubwa inawekezwa katika Level ya juu yaani kuanzia ngazi ya Wilaya na mikoa.

Ubora Wa Ukusanyaji Taarifa unatoa faida ya kiushindani katika kutoa Huduma Iliyobora Kama vile Upatikanaji wa Huduma ya matibabu na miundombinu yenye kuwezesha uharaka na Huduma inayokidhi mahitaji ya Wateja katika Eneo husika.

CHANZO CHA TAARIFA DUNI
S
erikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba inaongeza ubora Wa Taarifa kwenye Vyanzo vyake imejitahidi kuwekeza kwenye Mifumo mbali mbali kuhakisha mtoa taarifa(Secondary) anaingia kwenye mfumo na anatoa taarifa kwa wakati na zinatumika kwa wakati..(Nsmis)

  • Ukosefu wa Ujuzi kutoka kwa Watumishi wa Afya, Ni moja ya Tatizo kubwa linalopelekea kupatikana kwa taarifa ambazo siyo taarifa sahihi na siyo taarifa za wakati sahihi. Utakuta DNO(District nurse officer) Ni mbobezi katika taaluma yake, lakini Ni Duni katika masuala ya Tehama.
  • Mfumo wa Ukusanyaji Taarifa kutoka kwenye Vyanzo( Jamii, Mfano kutoka kwenye Kijiji, kitongoji na Kata) mtoa taarifa hawezi kuzingatia Umuhimu wa taarifa anayotoa kutokana na kwamba siyo mjuzi na hana Semina Elekezi au alipata Semina juu juu ambayo haiwezi kumsaidia kukusanya taarifa sahihi na kwa wakati. Mfano Taarifa za Taka na Mazingira( Waste Management system) taarifa hizo Ni Mara chache utakutana na taarifa sahihi maana mleta taarifa siyo mtu sahihi na hana Semina sahihi ambayo inaweza kumpa Umuhimu wa kuwa na taarifa sahihi.
  • Upikaji wa taarifa, utakuta taarifa zinachelewa kumfikia mtoa taarifa wa pili ambae Ni DHO(DISTRICT HEALTH OFFICER), Mkurugenzi (DED), AFISA MIPANGO AU Yeyote ambae Ni Mhusika ukizingatia, wakati huo anakuwa pushed kutuma taarifa kwenye mfumo, atafanya kulinganisha taarifa then zitatumika hizo hizo kwa ufanano huo huo au kwa upishano kidogo( No demand of improvement) kulingana na taarifa zilizo letwa.
  • View attachment 2292649
  • Ukosefu wa Dawati maalumu la taarifa za Afya kwenda kwenye mifumo, utakuta DHO AU DNO anataarifa na kazi zinamsubiri za kawaida, atajikuta taarifa zinakuwa nyingi na yeye Ni mtu mmoja na hawezi ajili mtu maana hana Fungu, itampasa kuingiza taarifa yeye Mwenyewe kitendo iko kitapelekea upatikanaji wa taarifa zenye nakosa mengi sana..baada ya kuandika M( MALE) ANAANDIKA (F) FEMALE, UREFU NI 21 ANAANDIKA 12 KUTOKANA NA UCHOVU.
NiNI KIFANYIKE
  1. Kusimamia mchakato wa utoaji taarifa kuanzia Katika ngazi ya Jamii (Kitongoji, mtaa) kwa MTOA HUDUMA WA JAMII(MUJA), hapa ndipo taarifa utoka na ndipo sehemu ambako hakuna usimamizi wa taarifa zinazopatikana, atapata Semina ya siku moja na kuendelea na Majukumu yake, huyu siyo mwajiriwa wa Serikali Ni mtu aliyechaguliwa na mkutano wa Kijiji kusaidia Hamasa ya huduma kwenye Jamii.
  2. Elimu ya ujuzi wa Tehama kwa Watumishi wa Afya Hasa hasa waliopo katika Mazingira ya kutoa taarifa katika mifumo ambayo ndio huchochea mapinduzi makubwa ya kisekta, Mfano ngazi ya Kata, ngazi ya Wilaya na ngazi mkoa, hapa ndipo taarifa sahihi zinatakiwa kutoka kulingana na mfumo wetu wa Afya.
  3. Uanzishwaji wa mifumo ambayo Ni rafiki kwa Watoa taarifa (Monitoring software and tools) kuhakikisha taarifa inayofika Ni taarifa mpya na yenye usahihi kutoka chanzo ngazi ya Jamii au Wilaya.
  4. Uzishwaji wa Dawati la Vyanzo vya taarifa za Afya kutoka kwenye ngazi ya Jamii Hadi ngazi ya Kata. Mchakato upitie kwa wataalumu ambao watasaidizana na Watoa Huduma kwenye ngazi ya Jamii kwa ajili ya upatikanaji wa taarifa sahihi zitakazo chochea mapinduzi ya Huduma Bora, miundombinu Bora na mipango Bora kwa ajili ya upatikanaji wa Huduma na kuokoa maisha ya watanzania wengi wanaopatikana katika Mazingira Duni..
  5. Ni Mnyororo wa Taarifa zinazotoka kwa WAVI(WATOA TAARIFA NGAZI YA JAMII) Wanapashwa kuwekewa utaratibu ambao Ni rasmi wa Malipo(Posho) kwa ajili ya kuongeza Motisha ya Wao kufanya kazi.
NAOMBA KUWASILISHA.

NB: NIMEKUWEKEA ATTACHMENT YA MOJA YA TAFITI zilizo wahi fanyika kuonyesha ukubwa wa Tatizo ili.. UDUNI WA DATA UNAVYOSABABISHA UDUNI WA HUDUMA ZA AFYA.
 

Attachments

Upvote 16
Naomba tuanze kulipigia Andiko hili Kura, maana Ni Andiko Bora na ambalo litaleta Tija iwapo litafanyiwa kazi.
 
Kabla ya 0 Kuna Kama kitufe bonyeza hapo nitakupa option mkuu.
 
Usitumie App nenda online..itakupa option
 

Attachments

  • Screenshot_20220715-194019.png
    Screenshot_20220715-194019.png
    46.6 KB · Views: 10
Kuna tatizo kwenye utaratibu wa. Kupiga kura, Sehemu ya kupigia kura siyo Rahisi Wala Haina option zaidi ya kutokukuruhusu kufanya hivyo.

Wahusika Tunaomba ufafanuzi Juu ya Tatizo ilo.
 
Kuna tatizo kwenye utaratibu wa. Kupiga kura, Sehemu ya kupigia kura siyo Rahisi Wala Haina option zaidi ya kutokukuruhusu kufanya hivyo.

Wahusika Tunaomba ufafanuzi Juu ya Tatizo ilo.
Kweli kabisa mkuu nashukuru umeliona hilo
 
Back
Top Bottom