Uduvi ndio kitu gani huko nyie watu wa Dar es Salaam?

Uduvi ndio kitu gani huko nyie watu wa Dar es Salaam?

View attachment 3189186
Watu wa Daslamu mna mambo mengi sana. Huu uduvi anaoubeza MKuu wa Mkoa ni kitu gani? Kuna mwanaJF humu anauza uduvi?
Kipi bora kuuza uduvi kwa kijana wa kiume au kuacha kuuza uduvi na kuwa panya road, mwizi, shoga n.k? Hivi nyie viongozi wa serikali mnataka nini? Mnahamasisha watu wajiajiri wakati nyie mmeajiriwa halafu wakishajiajiri mnawabeza kwa ajira zao eti unauza uduvi? Huyo anayeuza uduvi akija nyumbani kwa mkuu wa mkoa kila asubuhi atahudumiwa chai? Mchana atahudumiwa chakula cha mchana? Na jioni je, atahudumiwa chakula cha jioni? Viongozi acheni unaa. Mkishakalia hivyo viti msifikiri ndio mmemaliza kila kitu. Kuna maisha nje ya ukuu wa mkoa. Shubhaamit!
 
Upo sahihi mkuu ila tatizo lipo kwenye uwasilishaji,


Sidhani kama ni sahihi kusema kua ''Kijana wa kiume kuuza uduvi utaolewa''
au alikua ana maanisha nini kwa kusema hivyo?
Uwasilishaji wa namna hii ndio mzuri, ujumbe unamfikia mlengwa katika njia ya kuchoma kumoyo.

Angalia comments ndio utajua uwasilishaji ni mzuri, ila tatizo ni sosi wapokeaji wa kibongo, tumezoeshwa kubembelezwa.

Nilikuaga na bosi wangu mmoja ndio alikua type hizi, kulikuwa hakuna ujinga ujinga kazini.

Yaani eti kwa mfano uende kumpa umbea kuhusu mfanyakazi mwingine, usiombe siku mkutane wote watatu kwa pamoja(wewe, bosi, na huyo uliemchongea)

Yaani live bila chenga anakuita na anamwambia kila kitu muhusika mbele yako, kama ni shutuma atauliza ni kweli ama si kweli.

Kama ni kweli utaumbuka hapooo aibu nyingi, lakini alikua sio mtu wa kuweka kitu rohoni, wakishakusuta anaflash hapo hapo
 
Dagaa nyama wanaitwa hivyo
Huu ni uongo ,uduvi sio dagaa nyama
Huu hapa
Screenshot_20241231-112029.png
 
Back
Top Bottom