Upo sahihi mkuu ila tatizo lipo kwenye uwasilishaji,
Sidhani kama ni sahihi kusema kua ''Kijana wa kiume kuuza uduvi utaolewa''
au alikua ana maanisha nini kwa kusema hivyo?
Uwasilishaji wa namna hii ndio mzuri, ujumbe unamfikia mlengwa katika njia ya kuchoma kumoyo.
Angalia comments ndio utajua uwasilishaji ni mzuri, ila tatizo ni sosi wapokeaji wa kibongo, tumezoeshwa kubembelezwa.
Nilikuaga na bosi wangu mmoja ndio alikua type hizi, kulikuwa hakuna ujinga ujinga kazini.
Yaani eti kwa mfano uende kumpa umbea kuhusu mfanyakazi mwingine, usiombe siku mkutane wote watatu kwa pamoja(wewe, bosi, na huyo uliemchongea)
Yaani live bila chenga anakuita na anamwambia kila kitu muhusika mbele yako, kama ni shutuma atauliza ni kweli ama si kweli.
Kama ni kweli utaumbuka hapooo aibu nyingi, lakini alikua sio mtu wa kuweka kitu rohoni, wakishakusuta anaflash hapo hapo