UEFA Champions League kwenye Visimbuzi vya Dstv na Canal+

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Wakuu wa jukwaa, kama mnavyofahamu kesho ndio kesho. Usiku wa Ulaya unaanza kwa msimu huu. Mimi nimekuwa mdau wa mpira kwa muda mrefu, ila hawa Dstv wanakwama wapi? Mbona wenzao Canal+ wako na bei poa kwenye vifurushi vya soka.

Ili uweze kuona Mechi nyingi na unazotaka za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Dstv ni lazma uwe na kifurushi cha Compact Plus ambacho ni 84,000 wakati kwenye Canal+ ni mwendo wa kifurushi cha 40,000 tu unachagua utazame mechi unayotaka.

Siwapondi Dstv ila Wale mliolipa elfu 44 yaani compact mkitegemea mtapata mechi za Uefa poleni sana, bado mkaburu anajua kutunyonya. Kama hamjali lugha ya kifaransa tafuteni Canal+ mle maisha.

Kizuri kula na ndugu yako, kazi ni kwenu.
 
king'amuzi cha Canal+ nakipata wapi hapa dar na ni bei gani?
 
Mkuu unaweza nipa details za kuwapata canal+?
Niko mwanza uku pia wanazo offc? saiz nalipa compact+ japo wamepunguza bei ya kifurushi, ila naona canal+ wanabei rafiki Sana.
 
Jamaa wanajitahidi sema wanazidi kupigwa za uso na Azam malipo yao sio rafiki kwa wengi
Mkuu unalinganisha Azam na DStv kweli!, jaribu kuwa serious hata kidogo.

Hakuna watu wasiopenda vitu vizuri tatizo ni gharama tu,ndio maana nasisitiza ndugu zangu tutafute hela. Ukiwa na hela kila kitu kizuri kinakua ni affordable.
Sasa ona mtoa mada anakomalia kupata burudani kwa lugha ambayo haielewi, hii si adhabu kweli?
 
Kabisa Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…