carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limetumia barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), likitaka majibu kuhusu uongozi wa Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ikiwemo mradi wa FIFA Forward Enterprise (FFE) na tuzo ya Amani ya FIFA. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza vilivyoripoti Jumatatu, UEFA limetaka majibu hayo yatolewe kabla ya Novemba 2, 2026.
UEFA limekuwa mstari wa mbele kutaka Infantino ajiuzulu tangu alipopendekeza mradi wa FFE, ambao baadaye ulisitishwa. Mradi huo ulilenga kuanzisha kampuni ya kusimamia maslahi ya kibiashara ya mashindano ya FIFA, yakiwemo Kombe la Dunia, pamoja na kuuza sehemu ndogo ya hisa za kampuni hiyo kwa wawekezaji binafsi.
Infantino mwenye umri wa miaka 56, anayetarajiwa kugombea tena urais wa FIFA mwaka 2027, aliomba radhi kwa wajumbe wa Baraza la FIFA wiki iliyopita. Pia aliwataka kuwasilisha kwa maandishi maswali yoyote kuhusu namna anavyosimamia uongozi wa shirikisho hilo, akiahidi kuyajibu katika kikao kijacho cha baraza hilo kinachotarajiwa kufanyika Desemba 16, 2026.
Hata hivyo, Sky Sports na vyombo vingine vya habari vya Uingereza viliripoti Jumatatu kuwa Katibu Mkuu wa UEFA, Theodore Theodoridis, amemwandikia mwenzake wa FIFA, Mattias Grafstrom, akitaka majibu ya haraka kuhusu maswali 42 yanayohusu maeneo 12 ya uongozi wa shirikisho hilo.
Katika barua hiyo, Theodoridis amenukuliwa akisema maswali hayo yanahitaji majibu sasa na hayawezi kusubiri hadi kikao kijacho cha Baraza la FIFA
Chanzo : Reuters