UEFA mna chuki binafsi na Man United

loosimingori

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2017
Posts
920
Reaction score
1,145
Kama title hapo juu inavyojieleza.Mimi kama mshabiki wa majogoo wa jiji,jana usiku nilifadhaishwa mno na uamuzi wa UEFA kuifurusha man-U katika UCL kwasababu katika mechi ya mwisho ya UCL man city pia alipoteza 2-1 lakini UEFA imeivusha hadi nane bora.

Kitu ambacho kinafanya niseme man-U imeonewa na UEFA ni kwamba na wenyewe pia jana walipata kichapo cha 2-1 lakini cha kushangaza wenyewe wamefurushwa wakati matokeo hayo hayo yaliivusha man city hatua ya 8 bora.

Nafikiri jana united walidhani wangepata favor ya referee kama walivyopata upendeleo wa referee dhidi ya majogoo wa jiji na walivyocheza na chels.

Muhimu ni kwamba united msirely sana kwenye favor za marefarii kumbukeni kuwa champion league haichezeshwi na marefarii wa Uingereza pale mojawapo ya timu inayocheza ikiwa niya Uingereza
 
nlifikir umeandika kitu cha maana kumbe pumba tupu
 
Mungu alifanya makosa kukuumba
 
Mungu alifanya makosa kukuumba
mkuu hivi kweli MUNGU naye anakoseaga?MUNGU wetu uliyemuumbaji wa viumbe vyote tazama huyu kiumbe wako uliyemuumba kwa mfano wako anasema eti wewe MUNGU ulikosea kuniumba mm
 
washabiki wa EPL taratibu dawa ina anza kuwa ingia... tayari timu mbili zime toka kati ya timu tano... na ikitoka ya leo basi mtaendelea kusoma kuwa laliga ndio bora zaidi kwa miaka mingine miwili mbele...

Visca el Barca.... na mwaka huu lina baki tena Laliga... kuna kila dalili... kwa hizi timu hasa hawa wazee wa UCL Madrid, siwapendi ila ikifika huku huwa naungana nao tuna kuwa wazalendo...
 
Ma u ni kati ya timu ambazo ninafarijika sana ikifingwa,tena mvua ya magoli
 
Huu ni uvamizi sasa yani jukwaa limepata ugeni
 
Shabiki wa man u huyo amesha changanyikiwa hata hajui ameandika nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…