John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Champions League final) iliyokuwa imepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Krestovsky jijini Saint Petersburg Nchini Urusi imehamishwa na sasa itachezwa jijini Paris, Ufaransa.
Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limechukua maamuzi hayo kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.
UEFA imethibitisha maamuzi hayo asubuhi ya leo baada ya kikao cha dharura, kuwa fainali hiyo ambayo inatarajiwa kuchezwa Mei 28, 2022 badala ya kwenye uwanja wa awali ambao pia unajulikana kwa jina la Gazprom Arena kutokana na mapigano ambapo Urusi imeivamia Ukraine na kuanzisha mashambulizi ya kutumia silaha.