Habari,
Baada ya majeshi ya Urusi kuanza kuingia na kuvamia Ukraine siku chache zilizopita, UEFA imelazimika kuamisha mchezo wa fainali kutoka mji wa St Petersburg.
Mchezo wa fainali ya Mabingwa Wa Ulaya 2022 unatarajiwa kufanyika Paris baada ya St Petersburg kuondolewa kuwa muandaaji wa mchezo huo.
Maamuzi hayo yamekuja kutokana na kikao cha dharura kilichofanyika na mamlaka ya soka barani Ulaya kujaridi hali inavyoendelea baada ya Urusi kuvamia Ukraine.
Ilifahamika kuwa maamuzi ya kubadilisha muandaaji wa mchezo huo wa fainali hiyo yatatoka siku ya Alhamis baada tu ya Jeshi la Urusi kuingia Ukraine. Japo maamuzi hayo yalichelewa huku wakitafuta sehemu na kiwanja kitakachotumika kuchezea fainali hiyo.
Fainali imepangwa kuchezwa uwanja wa Stade De France mji wa Saint-Denis Tarehe 28 Mei 2022 saa 2000(GMT)
Nawasilisha Mzee Mkoloni.
Cc: Kichwa Kichafu.