UEFA yakanusha kutaka kuahirisha michezo kwa mwaka 1

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Chama cha soka Ulaya (UEFA) kimepinga madai kuwa kuna pendekezo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa linawataka waahirishe michuano yote ya kimataifa hadi mwishoni mwa mwaka 2021 kwa sababu ya corona.

UEFA inaamini hiyo sio sahihi kwa maana hiyo mpira utakuwa hauchezeki. Awali UEFA ilikubali kuahirisha michuano ya Euro 2020 baada ya kushauriana na WHO.

Msemaji wa UEFA alinukuliwa akisema si sahihi kwamba WHO wamependekeza mpira usichezwe hadi mwishoni mwa mwaka 2021.

WHO ndio walioishauri kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC) kuahirisha michuano yake kwa mwaka mmoja iliyokuwa ifanyike Tokyo na walishauri pia kuahirishwa kwa Euro 2020 kwa mwaka mmoja hadi 2021 sababu ya corona.
 
Maisha bila soka yametufanya sisi mateja wa soka kuwa sorber kifikra maana hatupati kitu roho inapenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…