UEFA yakataa ombi la msamaha la Infantino, yasisitiza mpango wa kususia kombe la dunia upo palepale

UEFA yakataa ombi la msamaha la Infantino, yasisitiza mpango wa kususia kombe la dunia upo palepale

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
UEFA isema katika taarifa yake kuwa ombi la msamaha la Rais wa FIFA, Gianni Infantino, halibadilishi kitu chochote, na kwamba vyama vyake wanachama 55 vinasalia kwenye msimamo wa mpango wao wa kususia Kombe la Dunia.

Soma Pia:
Taarifa hiyo inajiri siku moja baada ya uongozi wa FIFA kukutana nchini Morocco na kuthibitisha hadharani kuendelea kumuunga mkono Infantino, huku chombo hicho kinachosimamia soka duniani kikiomba msamaha kwa vyama vyake wanachama 211 kwa makosa yaliyojitokeza kwenye pendekezo lililofutwa la kuuza hisa za mustakabali wa kibiashara wa Kombe la Dunia.

Siku 5 zilizopita Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alitangaza kufuta rasmi mpango uliokuwa na utata mkubwa wa kuuza hisa za mashindano ya shirikisho hilo kwa wawekezaji binafsi.
 
Huyo bwana anaharibu kabisa mpira, hawezi kujaza timu nyingi hivyo kwenye kombe la dunia.

Kombe la dunia linapaswa kuwa na timu 32 tu na Afrika inatakiwa iwakilishwe na timu 5 tu na hii ni kulingana na kiwango kidogo cha soka katika bara hili.

Huyu bwana anataka mashindano hayo yashirikishe timu nyingi ili ajaze timu nyingi za Afrika kusudi wampatie kura nyingi wakati wa uchaguzi ili aendelee kuwa rais wa FIFA apige pesa.

Ni muda sasa FIFA inafaa kuwa na mihula ya uongozi na isizidi miwili tu ya miaka minne kila moja.
 
Balaa haya mambo ni magumu ngoja wasimame nayo
 
Hadi ajiuzulu ndo mambo yatakaa sawa, sasahivi haaminiki,tamaa ya pesa aliyonayo kama viongozi wa Afrika,anafanya maamuzi kama kipofu kabisaa.
 
CAF ni kusimama na Infantino tu, Jamaa anatubeba sana
Anatubeba kivipi huku wao wanaenda kupiga mabilioni ya pesa kwenye hilo dili halafu wengine wanaachiwa vichenji? Yeye kama rais wa FIFA anapaswa kuwajibika kwa mashirikisho yote ikiwemo ya Afrika, anachofanya sio hisani, ni wajibu wake. Akikosea akosolewe,hakuna cha anatubeba wala nini.
 
yeye ndie alietupa nafasi 10 za world cup, wazungu hilo jambo limewauma sana. tunatakiwa tuwe na shukurani.
 
yeye ndie alietupa nafasi 10 za world cup, wazungu hilo jambo limewauma sana. tunatakiwa tuwe na shukurani.
Nafasi kwenye world cup zingeongezeka automatically kama timu zetu zingekuwa zinafanya vizuri na kufika mbali kwenye michuano ya kombe la dunia bila hata hisani ya huyo Infantinno. Nafasi za kombe la dunia sio hisani, wanaofanya vizuri ndo wanapewa nafasi nyingi,badala ya kusubiri hisani ya Rais wa FIFA kwanini tusiboreshe timu zetu za taifa ili ziweze kufanya vizuri kwenye kombe la dunia? ikiwa kawaida timu za Afrika kufanya vizuri, nafasi zitakuja nyingi automatically kwa sababu tumestahili sio kama sasahivi tunasubiri hisani ya Infantino.
 
Back
Top Bottom