UEFA Zamani, sasa ni mfano tu.

Azarel

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
28,916
Reaction score
40,479
Habarini Wanamichezo.

Mimi si mkubwa sana wa Umri lakini Nina kumbukumbu nzuri sana ya soka ya kuanzia mwaka 1997.

Nina kumbukumbu ya tournaments mbalimbali mfano EPL na Champions league ya Ulaya (UEFA)

Nimekuwa nikisema mara kadhaa kuwa kuna aina flan flan ya Wachezaji ama Timu ambazo ni ngumu kuziona, kuzikuta katika miaka hii.

Ule Uzalendo, Useriousness na hata Ukakamavu na zaidi kumaintain kiwango stahiki ni TOFAUTI KABISA.

Kwa mfano, tazama Bayern Munich ya zamani, tazama Real Madrid ya kina Zidane au FC Porto tu ya zamani na sasa, sijui tatizo ni nini.

KWA MFANO, katika picha ifuatayo...ni kikosi cha AC MILAN ya Italia, hivi ni kwa vipi ambavyo hata Barcelona ya leo au Real Madrid angeweza kuifunga timu hii?

Hivi kweli Messi angeweza kumchenga na kumpita Gattuso, Cafu na Maldini akafunge?

Ni rahisi kumkaba na kuwazuia Shevchenko, Seedorf na kaka kufunga?


Naomba Tafakari yenu Wadau...hasa Wakongwe kwenye soka.
 
Kila time na moments zake. Kila Eufa ni nzuri kwa kipindi chake. Sijui Messi angempita Gatusso hutakaa upate jibu maana kila mmoja kacheza wakati tofauti.
Enjoy soccer Bwana. Tukutane tarehe 22/10,23/10.Fainali yangu ya kwanza kuangali ni pale Man united walifanya come back na ndo chanzo mimi kuwa shabiki wa Man united. Sijaacha kuangalia UEFA CL tokea kipindi hicho na ninaenjoy kila moments.
 
Dunia iko speed sanaa,,

Mambo yanabadilika nyanja zote sio tu soka, ukienda ktk Mzik ni ivo, ukirudi ktk siasa, pia ukicheki ktk kiuchumi mambo yako [emoji91],

Hata mtaa unaoishi tayar ushabadilika,, ukirudi unaonekana we ndo mgeni,, hii kitu huwez kuzuia,,

Kila Zama na kitabu chake[emoji3],

Siku hizi si umeona unaopoa kirahisi[emoji534], sio enzi zile uandike barua unasubiri majibu[emoji39]
 
zamani timu nyingi zilikuwa na uwezo wa kuwamiliki wachezaji wenye vipaji ndio maana haikuwa ajabu kuzikuta timu kama bayern leverkusen, valencia, dortmund, fiorentina, stuttgart, deportivo na nyenginezo kujaza mastar kwenye timu zao jambo lililopelekea kuzidi kwa ushindani wa timu.
kwa ufupi hapakuwepo na utofauti mkubwa sana ndani ya uwanja kati ya tabaka tajiri na tabaka masikini.


nyakati hizi hali imekuwa tofauti kwa sababu timu zenye kipato ndio zenye nguvu zaidi ya kutafuta wachezaji wenye vipaji ndio maana si ajabu kukuta timu moja inafuzu robo final ya champions league miaka 6 mfululizo.
huwezi kumkuta mchezaji kama sebastian veron anachezea timu kama lazio kwa sasa.

 
Mambo yanabadilika kiongozi ni kweli hio miaka timu za Italy zilikua moto sana hata Milan derby pale Sansiro kati ya Inter milan na Ac milan ilikua kubwa na maarufu kuzidi El Classico.

Ila saivi ligi ya Italy imekua ya timu moja tu kama vile France na Germany
 
Hao hao AC Milan, Liver anapindua matokeo? Au umeamua tu kutukumbusha kua alikuwepo beki anaitwa Gattuso.
Msimu uliopita Messi ndo mchezaji aliyezifunga magoli mengi timu kubwa sita za uingereza japo hachezi uko. Ndo useme hao mabeki wangeweza kumzuia Messi.
Messi na CR 7 ndo wachezaji bora wa dunia wa muda wote, acha kuwafananisha na akina Kaka. Hao jamaa daraja lao ni tofauti kabsa.
 
[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]kuwaga serious basi.
Kila zama na watu wake. Kuna wakati utafika watakuja watoto wetu na picha za wakina Rashford na Lingard wakiwanasibu kama washambuliaji wazuri kupata kutokea United.

Zama ikipita imepita.
 
mkuu zamani wachezaji wengi walikua na vipaji vya kuzaliwa tofauti na saizi wachezaji wengi wa kutengenezwa hasa uingereza ndo wana hayo mambo.miaka ya nyuma tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwenye top10 wanaingia wachezaji wote wazuri mpaka wakikwambia uchague lazima uchemshe.
 
Kama Andrea Pirlor, Ronaldinho n.k
 
Sio kila zamani nzuri ila ukweli kwa upande wa soka ile game ya brazil na italy final ni bora sana na ile game ya man u na bayern ni bora sana na kwa sasa ziko bora zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…