UEFALONA: Maamuzi ya utata yaliyobeba Barcelona UEFA tangia mwaka 2005

Unajua Barca wametengeneza kautaratibu fulani hivi ka kutaka kuaminisha watu ni timu bora zaidi kuwahi kutokea duniani lakini sijui kama ni makusudi au bahati mbaya ni kama wanafaidika na 'sympathy' fulani ya kitaasisi. Watu wengi na viongozi wengi wa soka duniani wamekuwa na kaupofu fulani hivi in favour ya Barcelona kiasi kwamba ni ngumu kuhukumu against wao. Mimi naamini mpira 'mwingi' wa Barcelona umelevya dunia kiasi cha kuona wao wako sahihi kwa kila kitu.

Mfano, kwa karibu miaka 10 hivi sikumbuki kuwahi kuona Barcelona ikiumizwa na makosa ya kile kinachoitwa bahati mbaya ya waamuzi kama zinavyoumizwa timu nyingine hadi katika mechi kubwa kabisa kama fainali za UEFA.

Pili, pamoja na Barcelona kucheza pasi nyingi lkn ikumbukwe hutumia nguvu kubwa kukaba wanapopoteza mpira, na wakati mwingine hutumia nguvu kubwa kupora mipira kutoka kwa wapinzani wao kiasi cha kuamini ni faulo lkn waamuzi huwa hawatoi faulo nyingi kwa timu pinzani, kinyume na wao Barcelona wakiguswa tu wakati mwingine timu pinzani ni kadi za njano kama njugu.
 
Umeandika vizuri, una hoja za nguvu. Ball possession ya Barcelona inawafanya wachezaji wa timu pinzani wacheze rafu. Barcelona pia ni wajanja wanapokuwa na mpira wanauburuza au kuuchezea mpira makusudi ili kumfanya mchezaji wa timu pinzani apatwe na mhemko na kufanya rafu.
 
Huu mtindo niliuona sana enzi za guardiola. Ilikua mchezaji wa barca akiwa na mpira halafu hajakabwa basi hatoi pass anasubiri hadi mchazaji wa tim pinzani anze kumkimbiza akimkaribia ndo atatoa pass. Hii ina faida mbili kwanza inatia hasira na kufanya mchezaji acheze rafu isiokua ya lazima. Pili inalazimisha wapinzani kutumia energy kubwa kukimbiza mipira ambayo hawawezi kuipata...hawa jamaa ni wajanja sana
 

Ni kweli kabisa, Guardiola alikuwa anawafundisha wachezaji wake mbinu za kuwafanya wapinzani wapate red cards. Kuna mchezaji mmoja alitoa siri hiyo, Guardiola alikasirika sana lakini mchezaji huyo hajajulikana mpaka leo. Hata ile ya Jumanne iliyopita kati ya Barcelona na Atletico Madrid, Busquests aliupata mpira katikati ya uwanja akawa hana haraka nao kama anasubiri kitu, ndipo Fernando Torres akamwendea 'kifala' na kumgonga Busquests nyuma ya goti. Refa hakuwa na jingine isipokuwa kutoa kadi ya njano ambayo ilikuwa ya pili na hivyo 'red card'.
 
Huyu sergio busquets ana cheat balaa nashangaa hawa marefa hawajamshtukia mpaka leo hii kwa faulu zake anazo fake, ndio maana kuna wasiwasi wa hawa jamaa kubebwa
 
Huyu sergio busquets ana cheat balaa nashangaa hawa marefa hawajamshtukia mpaka leo hii kwa faulu zake anazo fake, ndio maana kuna wasiwasi wa hawa jamaa kubebwa


Mimi nadhani marefa wanafahamu hilo siyo kwa Busquests tu bali kwa wachezaji wengi wa Barcelona. Kuna faulo nyingi sana wanazofanyiwa wachezaji wa Barcelona huwa hazionyeshwi kadi, na kama wangeonyesha kadi basi ni wazi wachezaji wengi wa timu pinzani wangekuwa wanatolewa nje.
 
kwani huwa hawatolewi nje? wnatolewa nje, na kama ni faulo ya kumtoa mtu nje kweli hapo hakuna tatizo lakini kuna maamuzi mengine hata mtu asiyejua sheria za mpira anaona hapa refa kapendelea
 
Nitaelezea zile Game nizikumbukazo vema kichwani.
-2009 Drogba ndo aliicost team, katika mpira kuna sehemu unatumia nguvu na akili. Drogba ni mchezaji mwenye nguvu sana akili pia, mtu kama Drogba kuanguka hovyo ndani ya 18 ni ngumu refa kuita Penalty, angekuwa Neymar, Hazard, Ronaldo, Messi n.k huenda tungeshuhudia Penalty siku ile.
-2010 Inter Milan iliingia uwanjani ikiwa na akili ya kupark Bus tuu, na ni kweli walizuia wote mpaka Samuel Eto'o. Mashambulizi kuelekea Golini kwao yalikuwa ni makali sana na wakaanza kutumia mbinu chafu ili kuwapunguz nguvu Barca, rejea hata Real Madrid, Chelsea, Atletico Madrid n.k wakitaka kuizima Barca na Messi wao ni lazima waingie uwanjani wakiwa na mbini chafu. Ni timu nzima kama sikosei ktk hii Game walibeba kadi za njano.

-2016 sio mara ya kwanza Atletico kuchukua kadi za njano nyingi akienda Camp Nou au akicheza na Real Madrid. Ni mtu asiyecheza mpira pekee ndiye atakayesema kuwa Toress kaonewa ktk ile kadi. Alishapewa kadi ya njano ya kwanza, akaja akacheza rafu kwa nyuma. Na rafu yoyote ukimchezea mtu kwa nyuma ni LAZIMA KADI ITOKE, wengine wakasema Toress alijikwaa, hivi toka lini mtu ukajikwaa mguu wa kulia na ukaangukia mguu huohuo?


HITIMISHO

- Kasi ya Barca kwa timu pinzani ni lazima iwape shida, tena saaana. Yaani kumzuia Messi, Iniesta, Alves, Busquets, Alba na kwa sasa kuna Neymar ni ngumu sana, unaweza ukaona ni rahisi kama hujawahi kuvaa viatu na kucheza mpira. Hawa jamaa style yao ya soka ni kali sana kwa timu pinzani.
 
kwani huwa hawatolewi nje? wnatolewa nje, na kama ni faulo ya kumtoa mtu nje kweli hapo hakuna tatizo lakini kuna maamuzi mengine hata mtu asiyejua sheria za mpira anaona hapa refa kapendelea

Sawa, comrade, masuala ya ushabiki na upenzi wa soka ni magumu...Katika debate inategemea mtu uko upande gani, ndiyo maana katika soka ni vigumu mtu kuwa neutral. Ni ngumu sana...Soka naifahamu, ila siwezi kusema kwa undani zaidi katika hili. Nakuthibitishia kuwa katika soccer, corruption iko nje nje. Na siyo Tanzania tu, hata Europe na hata kwenye mashindano ya FIFA iwe ni word cup au mashindano mengine...Ila katika debates za soka upenzi upo, PENALTI ya dhahiri kwa BARCELONA inaweza kuwa siyo PENALTI kwa REAL MADRID. Mchezaji amefanya faulo ya wazi na kupewa red card atabisha kwa refa na kuungwa mkono na wapenzi wa timu au klabu yake. Soka is a difficult game, ukiongoza soka ndipo utajua ugumu wa mchezo huu unaopendwa kuliko michezo yote duniani.
 
naelewa hayo mkuu, kuna ambazo zipo clear kabisa hapa ni kosa, kuna amabazo zipo 'debatable' au za mjaala yaani hakuna mwenye uhakika, na kuna ambazo zipo clear kabisa kwamba huyu kabebwa kacheki mechi ya barca vs chelsea 2009 , ukitazama kwa jicho neutral ni mfano mzuri kabaisa wa case niliyopiga red
 


sawa, comrade, nakubaliana na wewe ila kumbuka kuna human error pia.
 
wewe unatumia ushabiki zaidi kulio reason kwenye huu mjadala
 
Sasa ni battle of the purists hamna kubebana waliobaki hujui umetoka
 
At least red card mbili leo zingebidi zitolewe kwa wachezaji wa Barcelona,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…