Uelewe mfumo wa 3-4-3 anaotumia Antonio Conte

alitumia 3-5-2... na sio 3-4-3
Yes, ingawa mifumo yote ya kutumia mabeki 3 inahitaji nidhamu na ustadi mkubwa sana wa wachezaji nafikiri hili ndicho kilikosekana na babu wa watu akaamua kumwaga manyanga.

Kwa sasa tunaona wanatumia 4-2-3-1 na inayobadilika na kuwa 4-3-3 ; ingawa kuna shida bado kwenye wide players, sishangai kuona Jose Mourinho akiingia sokoni kutafuta word class wide players - fununu tu anataka kumnunua Payet na William January hii!! 🙂🙂🙂

Jose Mourinho ni shabiki mkubwa sana wa 4-3-3 iliyompa mafanikio makubwa sana Chelsea msiku wa kwanza na wa Pili alipofika England. Ilimsaidia kushinda back to back EPL hasa akiwatumia Demian Duff na Arjen Robben wakitokea pembeni.
 
mfumo huu ulianza baada ya kupigwa 3 na arsenal....huu mfumo umeruhusu goli moja tu...dhidi ya spurs
Yes mkuu, na uki add game ya juzi inakuwa ya nane tangu mfumo huu uanze kutumika huku chelsea ikiwa imetupia magoli 22 na wao kufungwa 2 tu.
 
Tafadhali sana mchezo mfumo huo huo mechi ya marudiano na Arsenal. Tungependa mno tuwagonge 3 zingine mkiwa na huo wazimu wenu.
 
Yes mkuu, na uki add game ya juzi inakuwa ya nane tangu mfumo huu uanze kutumika huku chelsea ikiwa imetupia magoli 22 na wao kufungwa 2 tu.
Kwa mfumo huo na wachezaji hao unawaza nini ukikutana na Madrid iliyo katika ubora wake
 
Kifupi huo mfumo hautaki mchezaji mzembe, mmoja kwa wote wote kwa mmoja.!
 
Conte akiwa Juventus kawatesa sana Inter milan,Ac Milan,Napoli,Roma...nk kwa kutumia huo mfumo hata kombe la Euro akiwa na Timu Ya Taifa katumia sana huo mfumo na Ukampa mafanikio hasa ukiwa na Beki zenye nidhamu kama Bonnucci,Chielini lazima wapinzani wapate shida tu.

Ila all in all antidote yake itapatikana soon kwa pale uingereza kuna timu Korofi sana pale
 
Mfumo huu ni dynamic, na ndiyo maana tunasema lazima uwe na wachezaji makini na wanaoelewa nini kinatakiwa kufanyika uwanjani na kwa wakati gani. Kwa mfano kama timu haina mpira basi mfumo huu hubadilika na kuwa 5 - 4 - 1
X6 na X7 wakishuka kuwa mabeki wa pembeni; wakati huo huo X11 na X9 wakishuka kuchukua nafasi zao kwenye midfield na wakiungana na X4 na X5. Timu ikiwa na mpira na inakwenda kushambulia basi mfumo huu unabadilika na kuwa
3 - 2 - 5 ; Engine za Kiungo yaani X6 (Alonso) na X7 (Moses) wanaungana na Kina Pedro, Costa na Hazard kusukuma mashambulizi huku wakiwa makini endapo timu itapoteza mpira kuwa makini wasikamatwe wakiwa off position. Mchezo mzuri wa kutumia akili - kosa moja na mchezaji ndiyo msiba kwa timu nzima.

Tunarudia kusema tena kwamba - so far so good kwa Conte - game ya 8 consecutive win's.
 
ni baada ya kipasuka na kipigo cha the gunners....ndio akaja na mfumo huo.......
 
ni uchambuzi mzuri sana, tafuta kituo cha redio mkuu utumie kipaji chako. Mwisho uwe unatembelea kule jukwaa la chelsea special thread .
 
Mfumo huu ni dynamic, na ndiyo maana tunasema lazima uwe na wachezaji makini na wanaoelewa nini kinatakiwa kufanyika uwanjani na kwa wakati gani. Kwa mfano kama timu haina mpira basi mfumo huu hubadilika na kuwa 5 - 4 - 1
X6 na X7 wakishuka kuwa mabeki wa pembeni; wakati huo huo X11 na X9 wakishuka kuchukua nafasi zao kwenye midfield na wakiungana na X4 na X5. Timu ikiwa na mpira na inakwenda kushambulia basi mfumo huu unabadilika na kuwa
3 - 2 - 5 ; Engine za Kiungo yaani X6 (Alonso) na X7 (Moses) wanaungana na Kina Pedro, Costa na Hazard kusukuma mashambulizi huku wakiwa makini endapo timu itapoteza mpira kuwa makini wasikamatwe wakiwa off position. Mchezo mzuri wa kutumia akili - kosa moja na mchezaji ndiyo msiba kwa timu nzima.

Tunarudia kusema tena kwamba - so far so good kwa Conte - game ya 8 consecutive win's.

Game ya kumi sasa Chelsea wanashinda, huu ni mchezo mzuri na pia ni mgumu sana, inahitaji uwe na wachezaji wenye mbio, wachezaji wenye kuweza kuhold mipira, na wachezaji wenye uwezo wa kukimbia na mipira

Ukiangalia mechi ya Sunderland nao waliingia na mfumo huohuo na hiyo mechi ilikuwa na watu nane katikati ya uwanja, Chelsea waliwazidi Sunderland kwenye wing ya kushoto (Alonso)

All in all mimi huwa nasema Chelsea ina wachezaji 15 uwanjani, saba wanakaba, saba wanashambulia na kipa mmoja, maana timu ikiwa kwenye pressure wale midfield wanne wanarudi kuungana na wale mabeki watatu na kufanya watu saba kuwa wanakaba na wale striker watatu wanarudi kuwa midfielders, na wakati wa kushambulia wale midfielder wanne wanaenda kutia nguvu mbele na wanakuwa wachezaji saba

Katika ile mechi ya Sunderland mpaka muda wa mapumziko kipa wa Chelsea alikuwa hajadaka mpira zaidi ya kupokea backpass na yeye kuwa kama mchezaji wa ndani

Wakiendelea hivi Chelsea wanaweza kuchukua kombe
 
Full time Eva 2 Vs 1 Arsenal
full time Eva 0 vs 5 Chelsea
tutakutana next Yr 2017 second leg.
Kwani Everton ndio kipimo chetu? Kwa hiyo unataka kuniambia second leg Diego Babu hatopakatwa na Mustafi Madevu sababu tu umemfunga Everton 5?

We mtamu tu babu, kampa ...utatupa tena. This time utakula 2 nyumbani kwako. Jiandae kupaki tupakue
 
Weka akiba ya maneno, hakuna jambo jipya chini ya jua. Huo mfumo au kushinda mechi 10 mfululizo ndio kitu kipya kwako?
 
Kwani Everton ndio kipimo chetu? Kwa hiyo unataka kuniambia second leg Diego Babu hatopakatwa na Mustafi Madevu sababu tu umemfunga Everton 5?

We mtamu tu babu, kampa ...utatupa tena. This time utakula 2 nyumbani kwako. Jiandae kupaki tupakue
Aya maneno yako yatunze tu naamini yatakurudia.next year.
00760cd32e8e779a740b5e6c2da1b69c.jpg
 
Back
Top Bottom