Utangulizi:Yapo maeneo mengi ya wazi ambayo kwa namna moja ama nyingine naona bado hayajapata bahati ya kuendelezwa ili kuweza kuwanufaisha wananchi wa maeneo hayo kutokana na faida zake. Kama maeneo haya ya wazi yataendelezwa, basi naamini kuwa yatasaidia sana wananchi kufanya tafakari za Maisha na kuburudika -kwa mfano uwekaji wa bembea ama bustani nzuri iliyooteshwa miti na maua
Lengo
- Kulinda maeneo ya wazi dhidi ya vitendo vya uzamizi ama kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa utupaji hovyo wa taka ama kama vituo vya ukusanyaji wa taka za majumbani
- Kuongeza mvuto kwenye maeneo ya wazi ili yawe rafiki kwa matumizi sahihi ya jamii badala ya kuachwa bila usimamizi thabiti
- Kukuza ubunifu kwa watu wanaopenda kuendeleza maeneo hayo ya wazi kwa mfano uwekaji wa bustani za maua ama viburudisho kama vile bembea ama migahawa ya juisi
- Kuongeza ajira rasmi, zenye heshima, zilizo ratibiwa kistaarabu na kutozwa kodi kwa njia sahiihi zaidi tofauti na biiashara za kuzagaa mtaani
- Kupunguza maeneo hatarishi na yasiyo salama kwa Watoto: lakini zaidi kuongeza maeneo ya kupunguza uwezekano wa watu kupata msongo wa mawazo
- Ili suala hili la uendeleza maeneo ya wazi likae vizuri, kuna umuhimu wa kukaa na jamii na wadau mbalimbali ili kujua wanawazia nini juu ya maeneo yao lakini pia kupata maoni ya watu wengine katika kupokkea ushauri. Makundi ya watu ya kuchota mawazo yao ni kama wanajamii, mipango miji, wafanya biashara, watu mashuhuri, taasisi na vikundi vya mazingira, wadau wa maendeleo
- Upatikanaji wa raslimali fedha za kufanikisha uendelezaji wa maeneo ya wazi yaliyo bainisha katika maeneo yote (kwa utaratibu wa kushirikiana kati ya Serikali na Sekta Binafsi)
- Ofisi ya Mkoa, Wilaya, Kata zihusishwe kwa ukaribu katika kuyatambua na kuyaboresha maeneo yote ya wazi katika jamii
- Kwa kuanzia, kila wilaya iandae orodha ya maeneo ya wazi, itengeneze miradi 2 mipya ya kuendeleza maeneo ya wazi: miradi ambayo itatekelezwa kila baada ya miezi 6
- Kupendezesha mji kwa kuongeza kitu cha tofauti matika makazi ya watu
- Kuongeza ajira rasmi kwa watu kujiajiri ama kuajiriwa na mradi
- Kumpa mwananchi maeneo ya kupumzika na kufurahia maisha peke yake ama na wengine
- Itasaidia katika utunzaji na kuongeza usafi wa mazingira
- Maeneo ya wazi yaliyoboreshwa yatasaidia wananchi kupunguza misongo ya mawazo
Upvote
2