SoC02 Ufadhili wa masomo unaotolewa na taasisi za nje unaakisi malengo/suluhisho la matatizo yetu Watanzania au ni mwendelezo wa ukoloni?

SoC02 Ufadhili wa masomo unaotolewa na taasisi za nje unaakisi malengo/suluhisho la matatizo yetu Watanzania au ni mwendelezo wa ukoloni?

Stories of Change - 2022 Competition

Wenger_tz

New Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Ndugu zangu,

Kuna taasisi na mataifa mengi ya nje ya nchi ambayo hutoa udhamini wa masomo ya juu katika kada mbalimbali ambazo nyingi hupatikana huko njee. Na kwakua udhamini huu wakat mwingine ni mzuri na unatuvutia wengi kutokana na kiwango cha fedha wanachotoa na huduma ambazo hupewa.

Wengi wetu tunaelewa kuwa moja ya sifa kuu katika kupata nafasi ya udhamini ni ufaulu wa juu sana Ukizingatia kwamba familia zetu nyingi nchini ni za hali ya chini lakini pia kwa utafiti usio rasmi vichwa(wenye uwezo wa juu shuleni) wengi hutoka katika familia hizi. Hivyo kwa kuzingatia hayo inakua ni rahisi kunasa kwenye huu mtego wa "full funded".

Taifa letu Tanzania lina changamoto nyingi mno , Maji, umeme miundombinu, huduma za afya zilizopitwa na wakati , uzalishaji mdogo wa chakula pamoja na upungufu wa thamani kwenye malighafi zetu.

Swali .
Je hizi nafasi wanaopewa vijana , na ndugu zetu wenye uwezo wa juu kielemu za udhamini wa masomo ambazo mara nyingi huwaelekeza na kada ya kusomea zinalenga kutatua changamoto zetu Tanzania?

Ninachoelewa mimi ni....
Kwanza; nafasi nyingi wanazotoa udhamini huwaelekeza watu kusoma kada ambazo ...

1. Zisizokua na manufaa katika kukabiliana na changamoto zetu watanzania mfano.. tourism, animal behaviour, administration, etc​
2 . Ukikuta ni katika zile kada zenye manufaa na sisi basi utakuta wanafundisha vitu vilivyo katika teknolojia ya juu kiasi kwamba kila kitu tutawategemea wao daima. Yaani wenyewe watajihakikishia soko la uhakika​

Wakati unakuta shida zetu hazihitaji technologia kubwa kiasi hicho,

Mfano , katika elimu za wenzetu wakiongelea namna ya kukabilina na magonjwa (kada yenye manufaa kwetu)
a)ni ngumu sana kusikia wanaongelea malaria,​
b)wakiongea kuhusu kudhibiti TB utasikia gene expert , angali kwetu ukigawa idadi ya hadubini nchi nzima kwa idadi ya watu unaweza kuta microscope 1 kwa watu laki mbili hapo hujaagusa hiyo gene expert​
3.ikiwa ni kada nzuri inayotulenga basi utakuta utafiti wako au msomo yako dhima yake inalenga sehemu yenye manufaa kwao au itakayowahitaji wao daima.​

Mfano. Unakuta kada inajina zurii( linaloonekana kulenga changamoto zetu) lakini mwisho unakuta in "rodents"

Unakuta mtu mwenye uwezo mkubwa kabisa amesomea biomedical engineering (uhandisi wa vifaa tiba ) mpaka hata PhD kasoma vifaa zaidi ya 500 lakin hospital anayofanya kazi ina pipettes na microscope labda na vingine viwil vitatu, kichwa mwake kuna technology ambayo itatufikia kikamilifu miaka 100 ijayo nayeye aliweka mkazo kwenye future technology kiasi kwamba hata mizani iliyo maabara ikiharibika nayeye huwa anaulizia kwa Fundi.

Naomba nieleweke kuwa sio kwamba hazina manufaa kwetu, hapana. Zina manufaa sana lakin haziendani na shida zetu na tukiendelea na mfumo tulionao itatuchukua miaka 200 kukabilia na changamoto tulizonazo. Ambazo kiuhalisia zinahitaji miaka mitano tu.

Taifa tuwe na mkakati wa kutatua shida zetu jamani, Tuwe na namna ya kupokea huu udhamini na kuuelekeza katika dira ya taifa letu.

Kama wasomi wetu watajiendeleza katika kada ambazo hazina msaada kwetu mwisho wa siku ndiyo unakuta tunasomea practical kwenye power points, na shida zetu zitakua soko la uhakika kabisa kwa ziada za watu wa nga'mbo.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom