Ufadhili wa Masomo ya Shahada ya Uzamili kwa Mwaka 2026/2027 Nchini Sweden

Ufadhili wa Masomo ya Shahada ya Uzamili kwa Mwaka 2026/2027 Nchini Sweden

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden unapenda kuutaarifu umma kuhusu fursa za ufadhili kamili wa masomo ya Shahada ya Uzamili unaotolewa na Taasisi ya Sweden (Swedish Institute – SI).

Ufadhili huu unatolewa katika zaidi ya programu 400 za masomo katika nyanja za utawala, afya ya umma, ujasiriamali na ubunifu, sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati na fani nyinginezo. Ufadhili huu ni wa malipo ya ada, posho ya kila mwezi pamoja na gharama za usafiri. Ubalozi unawahamasisha Watanzania wote wenye sifa stahiki kuomba ufadhili huu.

SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
ii. Awe ameomba au anaomba programu ya Shahada ya Uzamili inayostahiki kwa udhamini wa SI;
iii. Awe tayari kulipa ada ya maombi ya masomo kupitia mfumo wa udahili wa vyuo vikuu;
iv. Awe na uzoefu wa kazi unaothibitika;
v. Awe na uzoefu wa uongozi kutoka kwa mwajiri wa sasa au wa awali, au kupitia ushiriki katika asasi za kiraia.
IMG-20251215-WA0054.jpg
IMG-20251215-WA0057.jpg
 
Back
Top Bottom