Ufafanuzi hii Solidarity Fund ya Ndugu yetu Mwigulu!

Tengeneza Njia

Senior Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
121
Reaction score
205
Wakati bado waziri wetu wa fedha anaendelea kutapa tapa kwa vigugumizi akielezea mambo ambayo naamini hata yeye mwenyewe moyoni mwake anajua anatekeleza wajibu tu na si ukweli, tunaambiwa ni namna ya watu wengi, wananchi washiriki kwenye kuchangia SOLIDARITY FUND! - hebu nisaidieni ufafanuzi wa huu urojo?

Waziri anasema nchi ina miradi mikubwa na majukumu yameongezeka ya miradi mikubwa kama
bwawa la mwl.nyerere, reli, barabara za mikoa kwa mikoa, elimu, mikopo, elimu bure, afya,usambazaji wa umeme vijijini ndio maana imebidi wanyonye watanzania wanyonge ili pesa za miradi zipatikane.

Anasema, bila tozo maisha yao watoto wanyonge yasingeenda. Sidhani kama alichosema Mh. Mwigulu kina make any sense, sadly! unatambua tozo inaumiza ila tuendelee tu kuivumilia.
mnaumiza wananchi, gharama za maisha zimepanda (ninyi viongozi na familia zenu ham-experience haya) unatetea kuwa poleni wananchi endeleeni tu kutaabika kwa sababu hakuna namna nyingine ya kukusanya mapato zaidi ya kuwapokonya pesa ambazo tayari mnazo mifukoni kwenu!
Mishahara yenu mmeshaangalia namna inachangia umaskini wa watanzania wengi? Magari yenu? mikopo mliyokuwa mnasupport mnamwambia mama achukue - enzi za ndungai imefanya nini? Hamsemehi haya mambo mnatapa tapa tu na kudanganya umma!

Nyumbani Baba na Mama wakitaka kuanza miradi mipya ya familia (kufungua biashara ya familia, kununua gari n.k.) wazazi wanawapokonya watoto wao pesa walizonazo/ ambazo wanastahili kuwa nazo na kupunguza kuwahudumia na kuwapa haki zao kama watoto? - huu ni mfano mdogo tu! ipo mingi.
 
Walamba asali wanapoufurahia "ujinga" wetu

IMG_20220901_085859_867.jpg
 
Kupanga ni kuchagua. Kulikuwa na ulazima gani wa kufanya miradi hiyo kwa wakati mmoja wakati hali yetu tunaijua? Na kwa nini tulikazania kufanya miradi bila kufanya feasibility study? Na kwa nini tulikazania na bado tunakazania miradi ambayo tulishindwa kupata mikopo ya gharama nafuu kwa sababu taasisi za fedha za kimataifa ziliona hazina tija? Na kwa nini tulinunua ndege kwa pesa taslimu? Na tunaendelea kununua nyingine hata baada ya kujuq kuwa hazileti faida yeyote? Na kama hali ngumu kwa nini tunaendelea magari ya kifahari ambayo ununuzi na maintenance zake ni gharama kubwa? Na kuna wengine wameona hayatoshi sasa wanatumia helikopta! Watu wanacholalamika ni ile kuona haya machungu yanawapata wao tu lakini waliowapa dhamana ya kuwaongoza ni kama hawahusiki.

Kiongozi mzuri anaonyesha mifano. Kabla ya kuongeza hizi tozo tungeambiwa serikali imefanya juhudi gani za kupunguza matumizi.

Amandla....
 
Nasema tena, Kwa rasilimali walizopigania wazee wetu, wakifufuka Leo na kuona vijukuu wao tunavyokamuliwa watatutkana na kuanzisha vita dhidi ya serikali
 
Naomba umuulize mwigulu kama kuna siku mshahara wake ulikatwa kodi aje hapa tuzungumze huo unyonge
 
Mwigulu ni heri angebaki kimya kuliko kudhihirisha kuvimbiwa kwa madaraka
 
Back
Top Bottom