Ufafanuzi juu ya hili la Vvu au hiv+

kasuku mtu

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
321
Reaction score
94
Asalamu waleykumu waungwana!poleni kwa majukumu waungwana.....

Kuna mtu kanijia juzi anadai yeye ni hiv+ na boy friend wake ni hiv- sasa yeye anahitaji mtoto na mtoto wake asiwe na virusi vya ukimwi ni njia gani zitafanikisha hili kwa kuzuia maambukizi kwa baba mtarajiwa na mtoto watake mzaa?
Madocta tupeni majibu basi yaliyekwenda shule na sisi tuwape elimu ndugu zetu.
Aksanteni
 
Hili linawezekana kabisa. Muambie aongee na mshauri nasaha wake wakati anaenda clinic na ataelimishwa taratibu za kufuata. Ni matumaini yangu kuwa mwenziwe anafahamu kuwa yeye dada ana hiv. Bila hivyo hawatasaidika.
 
kama ukipewa ushauri wa kitaalam hutaweza kuufikisha kama ulivyo as maana ya jambo hupotea kila linaposafiri.

ushauri wangu ni huu hapa aende akamwone daktari wake wa maswala ya uzazi kinga na mtoto watampa ushauri sahihi toka vinywani mwao, ana kwa ana.

BTW kuna upotoshaji mkubwa sana unaofanywa na watu wanaojidai ni madaktari wa mitaani ambao kiukweli mm siuafiki hata kidogo na huwa unaptosha sana sana hasa juu ya magonjwa ambukizi na namna ya kujikinga nayo na tiba zake. so please ni busaa ukatafuta mtaalam kwenye upande huu amweleze yeye.
 
Kuwa muwazi usaidiwe, SEMA UKWELI KAMA NI WEWE MWENYEWE,hakuna kunyanyapaana jukwaani.
 
Kuwa muwazi usaidiwe, SEMA UKWELI KAMA NI WEWE MWENYEWE,hakuna kunyanyapaana jukwaani.

kaka mimi tena kasuku mtu na mitoto yote niliyo kua nayo hapa mjini sina hata mpango wa kuongeza....ningelibwia tuu mi donge mpaka basi
 

Mwambie azingatie sana ushauri wa gfsonwin wa kutafuta wataalamu husika wa hilo eneo.

Kama nimekusoma vizuri, nadhani shida yake zaidi haipo sana kwenye maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, japo hilo linahitaji uangalizi wake na linawezekana.

Utata upo kwenye upatikanaji wa huo ujauzito kwa hao ndugu zetu ambao kwa mujibu wa maelezo yako mmoja ni negative na mwingine ni positive. Hapo nadhani wataalam wataendelea na nini cha kufanya, nilitaka kuona kama nimekupata msaada unaouhitaji.

Ubarikiwe
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…