Ibara ya 39 ibara ndogo ya 3 inayohusu Haki ya watu walio chini ya ulinzi inasema,''Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake'' kama rasimu hii itapita na kuwa katiba je Tanzania tutajitoa kwenye vyombo vya haki kama mahakama ya kimataifa ya ICC?